Zaburi 97
97
Utukufu wa enzi ya Mungu
1BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie,
Visiwa vingi na vifurahi.
2Mawingu na giza vyamzunguka,
Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake.
3 #
Dan 7:10; Hab 3:5 Moto hutangulia mbele zake,
Nao huwateketeza watesi wake pande zote.
4Umeme wake uliuangaza ulimwengu,
Nchi ikaona ikatetemeka.
5Milima iliyeyuka kama nta mbele za BWANA,
Mbele za Bwana wa dunia yote.
6Mbingu zimetangaza haki yake,
Na watu wote wameuona utukufu wake.
7 #
Kut 20:4; Law 26:1; Isa 37:18,19; Yer 10:14; Ebr 1:6 Na waaibishwe wote waabuduo sanamu,
Wajivunao kwa vitu visivyofaa;
Enyi miungu yote, msujuduni Yeye.
8Sayuni imesikia na kufurahi,
Binti za Yuda walishangilia,
Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.
9 #
Efe 1:21
Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu,
Juu sana kuliko nchi yote;
Umetukuka sana juu ya miungu yote.
10 #
Zab 101:3; Amo 5:15; Rum 7:15; 1 Sam 2:9; Mit 2:8; Dan 3:28 Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu;
Huwalinda nafsi zao watauwa wake,
Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.
11Nuru humwangazia mwenye haki,
Na furaha ni kwa wanyofu wa moyo.
12Enyi wenye haki, mfurahieni BWANA,
Na kulishukuru jina lake takatifu.
Currently Selected:
Zaburi 97: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.