YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 87

87
Shangwe ya kuishi Sayuni
Ya Wakorahi. Zaburi. Wimbo.
1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3 # Isa 60:1 Mambo makuu yanasemwa kukuhusu,
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi;
Wanasema, Huyu alizaliwa humo.
5 # Eze 48:35; Mt 16:18 Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa,
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye Juu
Atauimarisha.
6 # Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9 BWANA ataweka kumbukumbu, awaandikapo mataifa,
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao ngoma na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.

Currently Selected:

Zaburi 87: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in