Zaburi 76
76
Mungu wa Waisraeli – Mungu mkuu
Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.
1Katika Yuda Mungu amejulikana,
Katika Israeli jina lake ni kuu.
2Kibanda chake pia kiko Salemu,
Na maskani yake iko Sayuni.
3 #
Zab 46:9; Eze 39:9 Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,
Ngao, upanga, na zana za vita.
4 #
Eze 38:12
Wewe U mwenye fahari na adhama,
Toka milima ya mateka.
5 #
Isa 46:12; Zab 13:3; Yer 51:39 Wametekwa wenye moyo thabiti;
Wamelala usingizi;
Wala hawakuiona mikono yao
Watu wote walio hodari.
6 #
Kut 15:1; Nah 2:13; Zek 12:4 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.
7 #
Ayu 41:10; Nah 1:6 Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe;
Naye ni nani awezaye kusimama ukasirikapo?
8Toka mbinguni ulitangaza hukumu;
Nchi iliogopa, ikakaa kimya.
9Mungu aliposimama ili kuhukumu
Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
10 #
Kut 9:16
Maana hasira ya binadamu itakusifu,
Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
11 #
Mhu 5:4; Zab 68:29 Wekeni nadhiri na mziondoe
Kwa BWANA, Mungu wenu.
Wote wanaomzunguka wamletee hedaya,
Yeye astahiliye kuogopwa.
12 #
Zab 68:35
Yeye huzikata roho za wakuu;
Na kuwatisha wafalme wa dunia.
Currently Selected:
Zaburi 76: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.