Zaburi 6
6
Sala ya kuponywa ugonjwa hatari
Kwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi; kulingana na mtindo wa Sheminithi. Zaburi ya Daudi.
1 #
Zab 38:1
BWANA, usinikemee kwa hasira yako,
Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2 #
Hos 6:1
BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;
BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3 #
Mit 18:14; Mt 26:38 Na nafsi yangu imefadhaika sana;
Na Wewe, BWANA, hadi lini?
4BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5 #
Zab 30:9
Maana mautini hapana kumbukumbu lako;
Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6Nimechoka kwa kuugua kwangu;
Kila usiku nakibubujikia kitanda changu;
Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7Macho yangu yameharibika kwa masumbufu,
Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8 #
Mt 7:23; Lk 13:27 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;
Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
9 #
Zab 3:4; 31:22; 40:1,2 BWANA ameisikia dua yangu;
BWANA atayatakabali maombi yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
Watarudi nyuma, kwa ghafla wataaibika.
Currently Selected:
Zaburi 6: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.