YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 43

43
Sala kwa Mungu wakati wa shida
1 # Zab 7:8 Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki,
Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.
2 # Zab 28:7; Isa 26:4 Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?
Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
3 # Zab 2:6; 3:4 Nitumie nuru yako na kweli yako ziniongoze,
Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata katika maskani yako.
4Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye
furaha yangu na shangwe yangu;
Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
5 # Zab 42:5,11 Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu;
Maana nitamsifu tena,
Aliye msaada wangu,
Na Mungu wangu.

Currently Selected:

Zaburi 43: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in