YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 28

28
Sala ya kupata msaada na shukrani za msaada
Ya Daudi.
1Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu,
Usiwe kwangu kama kiziwi.
Nisije nikafanana nao washukao shimoni,
Ikiwa umeninyamalia.
2Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo,
Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
3Usinikokote pamoja na wasio haki,
Wala pamoja na watenda maovu.
Wawaambiao jirani zao maneno ya amani,
Lakini mioyoni mwao mna madhara.
4 # Ufu 22:12; 2 Tim 4:14 Uwape sawasawa na vitendo vyao,
Na kwa kadiri ya uovu wa matendo yao,
Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao,
Uwalipe kile wanachostahili.
5Maana hawazifahamu kazi za BWANA,
Wala matendo ya mikono yake,
Atawavunja wala hatawajenga tena;
6Na ahimidiwe BWANA.
Maana ameisikia sauti ya dua yangu;
7 # Zab 18:2 BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.
Moyo wangu umemtumaini,
Nami nimesaidiwa;
Basi, moyo wangu unashangilia,
Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
8BWANA ni nguvu za watu wake,
Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi#28:8 Au, mtiwa mafuta. wake.
9Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako,
Uwachunge, uwachukue milele.

Currently Selected:

Zaburi 28: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy