YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 149

149
Sifa kwa wema wa Mungu kwa Israeli
1 # Isa 42:10 Haleluya.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
2 # Ayu 35:10; Zek 9:9 Israeli na amfurahie Yeye aliyemwumba,
Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.
3Na walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.
4 # Mit 11:20 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,
Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5Watauwa na waushangilie utukufu,
Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.
6 # Kum 7:1-2; Ebr 4:12; Ufu 1:16 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,
Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.
7Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,
Na adhabu juu ya makabila ya watu.
8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,
Na wakuu wao kwa pingu za chuma.
9 # Kum 7:1-2; Ufu 5:10; Rum 16:20; 1 Yoh 5:4 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa;
Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.
Haleluya.

Currently Selected:

Zaburi 149: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in