YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 116

116
Shukrani kwa kuponywa maradhi
1Haleluya.
Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza
Sauti yangu na dua zangu.
2Kwa maana amenitegea sikio lake,
Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.
3Kamba za mauti zilinizunguka,
Shida za kuzimu zilinipata.
Nilipata dhiki na mateso;
4Nikaliitia jina la BWANA.
Ee BWANA, nakuomba sana,
Uniokoe nafsi yangu.
5 # Ezr 9:15; Neh 9:8; Zab 11:7; Yer 12:1; Omb 1:18; Ufu 16:5 BWANA ni mwenye neema na haki,
Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.
6BWANA huwalinda wasio na hila;
Nilidhilika, akaniokoa.
7 # Yer 6:16; Mt 11:29 Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako,
Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.
8Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,
Macho yangu na machozi,
Na miguu yangu na kuanguka.
9Nitaenenda mbele za BWANA
Katika nchi za walio hai.
10 # 2 Kor 4:13 Nilidumisha imani yangu, hata niliposema,
Mimi nateseka sana.
11 # 2 Fal 4:16; Yer 9:5; Rum 3:4 Nikiwa katika hangaiko langu nikasema,
Wanadamu wote ni waongo.
12Nimrudishie BWANA nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
13Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la BWANA;
14 # Zab 22:25; Yon 2:6 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,
Naam, mbele ya watu wake wote.
15 # Ayu 5:26; Zab 72:14; Lk 16:22; Ufu 14:13 Kifo cha waaminifu wa Mungu,
kina thamani machoni pa BWANA.
16Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako,
Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako,
Umevifungua vifungo vyangu.
17Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la BWANA;
18Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,
Naam, mbele ya watu wake wote.
19Katika nyua za nyumba ya BWANA,
Ndani yako, Ee Yerusalemu.

Currently Selected:

Zaburi 116: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy