Mithali 18
18
1Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe;
Hushindana na kila shauri jema.
2Mpumbavu hapendezwi na ufahamu;
Ila moyo wake udhihirike tu.
3Ajapo asiye haki, huja dharau pia;
Na pamoja na aibu huja lawama.
4 #
Zab 78:2
Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi;
Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.
5 #
Law 19:15; Kum 1:17; Ayu 13:7,8; Mit 24:23 Kukubali uso wake asiye haki si vizuri;
Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.
6Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina,
Na kinywa chake huita mapigo.
7Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake,
Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
8Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo;
Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
9Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake,
Ni ndugu yake aliye mharibifu.
10 #
2 Sam 22:3,51; Zab 18:2 Jina la BWANA ni ngome imara;
Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
11Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;
Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.
12Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna;
Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
13Yeye ajibuye kabla hajasikia,
Ni upumbavu na aibu kwake.
14Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake;
Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?
15 #
Efe 1:17
Moyo wa mwenye busara hupata maarifa;
Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.
16 #
Mwa 39:2-6; 41:14,38-44; Dan 1:17-20; 6:3 Zawadi ya mtu humpatia nafasi;
Humleta mbele ya watu wakuu.
17Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki;
Lakini jirani yake huja na kumchunguza.
18Kura hukomesha mashindano;
Hukata maneno ya wakuu.
19Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu;
Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.
20Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake;
Atashiba mazao ya midomo yake.
21 #
Mt 12:37
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;
Na wao waupendao watakula matunda yake.
22Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
23 #
Mwa 42:13-16; Yak 2:3 Maskini hutumia maombi;
Bali tajiri hujibu kwa ukali.
24 #
Yn 15:14,15 Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe;
Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
Currently Selected:
Mithali 18: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.