YouVersion Logo
Search Icon

Filemoni UTANGULIZI

UTANGULIZI
Waraka huu wa Paulo kwa rafiki yake Filemoni (1:17) una nafasi ya pekee katika Nyaraka zote za Agano Jipya. Ni Waraka mfupi kuliko Nyaraka zote za Paulo na, tofauti na Nyaraka zake nyingine, huu ni wa binafsi kabisa. Mlengwa wa Waraka huu ni mtu aitwaye Filemoni. Kwa kuwa Onesimo, mtumwa wa Filemoni, anatajwa mahali pengine kama mwenyeji wa Kolosai (Kol 4:9) kama vile Arkipo ambaye anatajwa katika sehemu ya salamu ya Waraka huu (aya 2), wengi wanafikiri kwamba Filemoni naye pia alikuwa mwenyeji wa Kolosai. Lakini wengine wanafikiri alitoka Efeso. Filemoni alikuwa mtu maarufu na mkarimu ambaye labda alipata kuwa Mkristo kwa njia ya Paulo (aya 19) na kanisa lilikutana nyumbani kwake (aya 2).
Kwa kuwa Paulo aliwajua vizuri Filemoni na Onesimo aliandika Waraka huu ili kumsihi Filemoni ampokee tena mtumwa wake yaani Onesimo. Paulo anamwomba ampokee sio kama mtumwa aliyetoroka tu bali ndugu katika Kristo.
Waraka huu kwa Filemoni unaonesha jinsi Paulo alivyoweza kutumia hali mpya ya Kikristo kukabili hali ya utumwa wa mtu kwa mtu mwingine wakati kimsingi hakuna mtu aliye mtumwa wa mtu mwingine na kwamba Wakristo ni ndugu katika kuungana na Bwana. Paulo anatarajia kwamba Filemoni atampokea huyo mtumwa wake mtoro kwa njia inayoonesha maisha mapya ya Kikristo, tena Paulo yuko tayari kulipa chochote ambacho Onesimo alikuwa amechukua kutoka kwa Filemoni.

Currently Selected:

Filemoni UTANGULIZI: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in