YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 9

9
Pasaka katika Sinai
1 # Kut 12:1-13 Kisha BWANA akanena na Musa katika bara ya Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka kwao katika nchi ya Misri, akamwambia, 2#Kut 12:1; Law 23:5; Kum 16:1,2; Hes 28:16; Ebr 10:1 Tena, wana wa Israeli na waadhimishe sikukuu ya Pasaka kwa wakati wake ulioagizwa. 3Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, wakati wa jioni, mtaiadhimisha kwa wakati wake ulioagizwa; kwa amri zake zote, na kama hukumu zake zote zilivyo, ndivyo mtakavyoisherehekea. 4Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waadhimishe sikukuu hiyo ya Pasaka; 5#Yos 5:10 Nao wakaiadhmisha Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.
6 # Hes 5:2; 6:6,7; Yn 18:28; Kut 18:15; Hes 27:2 Basi walikuwako wanaume kadhaa waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia, 7#1 Kor 5:7,8 Sisi tuko katika hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli? 8#Zab 25:14; 85:8; Yn 7:17; Efe 1:9,18; Ebr 3:5,6 Musa akawaambia, Ngojeni hapo; hata nipate sikiza BWANA atakaloagiza juu yenu.
9BWANA akanena na Musa, akamwambia, 10Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, yeyote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA; 11#2 Nya 30:2,15; Kut 12:8 mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni,#9:11 Katika Kiebrania ni ‘katikati ya jioni’. wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; 12#Kut 12:10,43,46; Yn 19:36 wasisaze kitu chake chochote hadi asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika. 13#Mwa 17:14; Kut 12:15; Law 17:4; Ebr 6:6; 12:25; Hes 5:31; Gal 3:10; Ebr 10:26 Lakini mtu aliye safi, wala hakuwa katika safari, naye amekosa kuishika Pasaka, mtu huyo atatengwa na watu wake; kwa sababu hakumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioamriwa, mtu huyo atachukua dhambi yake. 14#Kut 12:49 Na kama mgeni akiketi kati yenu ugenini, naye ataka kuishika Pasaka kwa BWANA; kama hiyo sheria ya Pasaka ilivyo, na kama amri yake ilivyo, ndivyo atakavyofanya; mtakuwa na sheria moja, kwa huyo aliye mgeni, na kwa huyo aliyezaliwa katika nchi.
Wingu la moto
15 # Kut 13:21 Na siku hiyo maskani iliposimamishwa, lile wingu likaifunika maskani, yaani, hema ya kukutania; wakati wa jioni likawa juu ya maskani, mfano wa moto, hata asubuhi. 16#Kut 13:21,22; 40:34; Kum 1:33; Neh 9:12 Ndivyo ilivyokuwa sikuzote; lile wingu liliifunika kwa mfano wa moto usiku. 17#Kut 40:36,37; Hes 10:11,33,34; Zab 78:14; 80:1; Isa 49:10; Yn 10:4 Na kila lilipoinuliwa lile wingu juu ya ile Hema ndipo wana wa Israeli waliposafiri; na mahali lilipokaa lile wingu, ndipo wana wa Israeli walipopiga kambi yao. 18#1 Kor 10:1 Kwa amri ya BWANA Wana wa Israeli walisafiri, na kwa amri ya BWANA walipiga kambi; wakati lile wingu ilipokaa juu ya maskani walikaa katika kambi yao. 19Hata lile wingu lilipokawia juu ya maskani siku nyingi, wana wa Israeli walimtii BWANA, na hawakusafiri. 20#Zab 48:14; Mit 3:5,6 Na pengine lile wingu lilikaa juu ya maskani siku chache; ndipo kwa amri ya BWANA walikaa katika kambi yao, tena kwa amri ya BWANA walisafiri. 21#Mt 28:20 Na pengine lile wingu lilikaa tangu jioni hata asubuhi; na lile wingu lilipoinuliwa asubuhi walisafiri, au kama likikaa usiku na mchana pia, lilipoinuliwa lile wingu, ndipo waliposafiri. 22#Kut 40:36,37; Zab 73:24; 107:7; Isa 63:14 Ikiwa lile wingu lilikawia, likikaa juu ya maskani siku mbili, au mwezi, au mwaka, wana wa Israeli walikaa katika kambi yao, wasisafiri; 23#Zab 73:24; 107:7; Isa 63:14 bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; walimtii BWANA, kwa mkono wa Musa.

Currently Selected:

Hesabu 9: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in