YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 7

7
Sadaka za viongozi
1 # Mwa 32:26,29; 1 Fal 8:64; 1 Nya 4:10; Mt 23:19; Efe 1:3 Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa; 2#Kut 35:27; 1 Nya 29:6-8; 2 Nya 35:8; Ezr 2:68,69; Neh 7:70-72 ndipo wakuu wa Israeli, vichwa vya nyumba za baba zao, wakatoa matoleo; hao ndio wakuu wa makabila, hao ndio waliokuwa juu yao waliohesabiwa; 3nao wakamletea BWANA matoleo yao, magari sita yenye mafuniko juu, na ng'ombe kumi na wawili; gari moja kwa wakuu wawili wawili, na ng'ombe mmoja kwa kila mkuu; nao wakayasongeza hapo mbele ya maskani. 4Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 5Pokea mikononi mwao, ili kwamba viwe vya kutumiwa katika utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawapa Walawi vitu hivyo, kila mtu utampa kama utumishi wake ulivyo. 6Basi Musa akapokea hayo magari, na ng'ombe, akawapa Walawi. 7Wana wa Gershoni akawapa magari mawili na ng'ombe wanne, kama utumishi wao ulivyokuwa; 8na wana wa Merari akawapa magari manne na ng'ombe wanane kama utumishi wao ulivyokuwa, chini ya mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni kuhani. 9#1 Nya 15:3,13; 23:26; 2 Sam 6:13 Lakini hakuwapa wana wa Kohathi; maana, utumishi wa vile vitu vitakatifu ulikuwa ni wao; nao wakavichukua mabegani mwao. 10#Kum 20:6; 1 Fal 8:63; Ezr 6:16 Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu. 11#1 Kor 14:33 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, Watasongeza matoleo yao, kila mkuu kwa siku yake, kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.
12Basi aliyetoa matoleo yake siku ya kwanza ni Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda; 13#Kut 25:29; Ezr 1:9,10; 8:25; Yer 52:19; Dan 5:3 na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga; 14#2 Fal 25:14,15; Kut 30:34; 37:29; Law 16:12,13; Hes 16:46,47; Kum 33:8,10; Zab 141:2; Isa 60:6; Yer 6:20; 41:5; Eze 16:18; Mal 1:11; Ufu 5:8; 8:3,4 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 15ng'ombe dume mchanga, mmoja na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 16#Law 4:23 mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; 17#Lk 3:32 na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
18Siku ya pili Nethaneli mwana wa Suari, mkuu wa Isakari, alitoa; 19yeye akasongeza matoleo yake, sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa ni sadaka ya unga; 20na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilikuwa kimejaa uvumba; 21#Mwa 8:20; Law 6:9; Zab 20:1-3; 51:19; Efe 5:2; Ebr 9:13 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 22na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; 23#Law 7:11,13; 1 Fal 8:63; Mit 7:14; Kol 1:20 na kwa dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Nethaneli mwana wa Suari.
24Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zabuloni; 25matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 26na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 27#Isa 53:7; Yn 1:29; Mdo 8:32; Gal 1:4; 1 Pet 1:19; 2:24; Ufu 5:6-14; 13:8 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 28na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 29tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Eliabu mwana wa Heloni.
30Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, mkuu wa wana wa Reubeni; 31matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 32na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 33na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 34na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 35tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Elisuri mwana wa Shedeuri.
36Siku ya tano Shelumieli mwana wa Suri-shadai, mkuu wa wana Simeoni; 37matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 38na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 39#Kut 12:5; Yn 1:29; Ebr 9:28; 1 Pet 3:18; Ufu 5:6 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 40na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 41tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Shelumieli mwana wa Suri-shadai.
42 # Hes 1:14; 2:14 Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, mkuu wa wana wa Gadi 43#Law 2:5; 14:10; Ebr 1:9; 1 Yoh 2:27 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 44na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 45#Zab 40:6; 51:16; Isa 1:11; 53:4; Yer 7:22; Amo 5:22; 2 Kor 5:21 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 46na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 47tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Eliasafu mwana wa Deueli.
48 # Hes 1:10; 2:18; 1 Nya 7:26 Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efraimu; 49matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 50#Kum 33:10; Zab 66:15; 141:2; Lk 1:10; Ufu 5:8; 8:3 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 51#Mik 6:6-8 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, wa sadaka ya kuteketezwa; 52na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 53tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Elishama mwana wa Amihudi.
54 # Hes 1:10; 2:20 Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, mkuu wa wana wa Manase; 55matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 56#Kut 30:7 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 57#Kut 12:5; Yn 1:29; Mdo 8:32; 1 Pet 1:19; Ufu 5:6 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 58na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 59#Law 3:1; Mik 5:5; 2 Kor 5:19,21; Efe 2:14 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.
60Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, mkuu wa wana wa Benyamini; 61#Hes 1:11; 2:22 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 62#Isa 66:20; Zab 141:2; Dan 9:27; Rum 15:16; Flp 4:18; Ebr 13:15; Ufu 5:8; 8:3,4 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 63#Zab 40:6; Isa 53:4; 2 Kor 5:21 na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 64na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 65#Law 3:1; 1 Fal 8:63; Mit 7:14; Eze 45:17; Kol 1:20 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Abidani mwana wa Gideoni.
66 # Hes 1:12; 2:25 Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, mkuu wa wana wa Dani; 67#Law 27:25; Hes 3:47; Kut 30:13 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 68#Kut 30:7-9; Hes 16:35; Zab 141:2; Isa 66:20; Dan 9:27; Mal 1:11; Lk 1:9; Rum 15:16; Flp 4:18; Ebr 13:15 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 69na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 70na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 71tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.
72 # Hes 1:13; 2:27 Na siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, mkuu wa wana wa Asheri; 73matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 74#Mal 1:11; Lk 1:11 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 75na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 76na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 77tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Pagieli mwana wa Okrani.
78 # Hes 1:15; 2:29 Na siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, mkuu wa wana wa Naftali; 79#Ezr 1:9,10; Yer 52:19; Dan 5:2; Zek 14:20; Mt 14:8,11 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga; 80na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba; 81na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 82na mbuzi dume mmoja kwa sadaka ya dhambi; 83tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Ahira mwana wa Enani.
84 # 1 Kor 1:13; Ezr 2:68; Neh 7:70; Isa 60:6,10; Ebr 13:10; Ufu 21:14; Amu 5:9; Yos 22:13,14; Mit 17:7; Hos 13:10 Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili; 85kila sahani ya fedha uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na kila bakuli uzani wake ni shekeli sabini; fedha yote ya vile vyombo ilikuwa shekeli elfu mbili na mia nne, kwa shekeli ya mahali patakatifu; 86#Kut 30:13 na vijiko vya dhahabu vilivyojaa uvumba kumi na viwili, uzani wake kila kijiko shekeli kumi, kwa shekeli ya mahali patakatifu; dhahabu yote ya vile vijiko ilikuwa shekeli mia moja na ishirini; 87#Rum 12:1; Law 2:1; 9:17; Hes 15:4 ng'ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng'ombe dume kumi na wawili, na hao kondoo dume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi dume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili; 88na ng'ombe wote waliokuwa wa dhabihu ya sadaka za amani ni ng'ombe dume ishirini na wanne, na hao kondoo dume walikuwa ni sitini, na hao mbuzi dume walikuwa ni sitini, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa sitini. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, baada ya hiyo madhabahu kutiwa mafuta.
89 # Kut 31:18; 33:9; 34:3,9; Hes 11:17; 12:8; Kut 25:22; Law 1:1; Ebr 4:16; Mwa 3:24; 1 Fal 6:23; Zab 18:10; 99:1; Ebr 1:14; 9:5 Kisha, Musa alipoingia ndani ya hema ya kukutania ili kunena na Mungu#7:89 Katika Kiebrania ni kunena ‘naye’. ndipo alipoisikia Sauti ikinena naye kutoka hapo juu ya kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, ikitoka kati ya yale makerubi#7:89 Katika Kiebrania ni viumbe wawili wenye mabawa. mawili; naye akanena naye.

Currently Selected:

Hesabu 7: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in