YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 26

26
Hesabu ya kizazi kipya
1 # Hes 1:1-46 Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia, 2#Kut 30:12; 38:25; Hes 1:2 Fanya hesabu ya jumuiya yote ya wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani. 3#Kum 4:46-49; 34:1 Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia, 4Fanyeni hesabu ya watu, kuanzia umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri.
5 # Mwa 29:32; 46:8; 1 Nya 5:1; Ufu 7:5 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu; 6na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi. 7Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tatu, mia saba na thelathini. 8Na wana wa Palu; Eliabu. 9#Hes 16:1,2; 27:3; Kum 11:6; Isa 65:16; Zab 106:17; Yud 1:11 Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA; 10#Hes 16:38; 1 Sam 2:34; Ayu 31:3; Zab 145:20; Yer 29:22; 1 Kor 10:6; 2 Pet 2:6; Yud 1:7 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara. 11#Kut 6:24; 1 Nya 6:22; Eze 18:20 Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa.
12 # Mwa 46:10; Kut 6:15; 1 Nya 4:24 Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini; 13#Mwa 46:10 wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli. 14Hawa ndizo jamaa wa Wasimeoni, watu elfu ishirini na mbili na mia mbili.
15Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni; 16wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri; 17#Mwa 46:16 wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli. 18Hawa ndio jamaa wa wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, elfu arubaini na mia tano.
19 # Mwa 38:2; 46:12; 1 Nya 2:3 Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani. 20#Mwa 49:8; Ufu 7:5 Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera. 21Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli. 22Hawa ndio jamaa wa Yuda kama waliohesabiwa kwao, elfu sabini na sita na mia tano.
23 # Mwa 46:13; 49:14 Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva; 24wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni. 25Hawa ndio jamaa wa Isakari kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na nne na mia tatu.
26 # Mwa 46:14; 49:13 Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli. 27Hawa ndio jamaa wa Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na mia tano.
28 # Mwa 41:51; 46:20; 48:3,13-20 Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu. 29#Hes 32:39; 36:1 Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi. 30#Yos 17:2 Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki; 31na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu; 32na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi. 33#Hes 27:1; 36:11; Yos 17:3 Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na watoto wa kiume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza. 34Hawa ndizo jamaa wa Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni elfu hamsini na mbili na mia saba.
35 # 1 Nya 7:20 Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi. 36Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani. 37#Kum 33:13-17 Hawa ndio jamaa wa wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, elfu thelathini na mbili na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao.
38 # Mwa 46:21; 1 Nya 7:6; 8:1 Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu; 39#Mwa 46:21; 1 Nya 7:12 wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu. 40#1 Nya 8:3 Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani. 41Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia sita.
42 # Mwa 46:23; 49:16; Hes 1:38,39; Kum 33:22 Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao. 43Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne.
44 # Mwa 46:17; 1 Nya 7:30 Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia. 45Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli. 46Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera. 47Hawa ndio jamaa wa wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, elfu hamsini na tatu na mia nne.
48 # Mwa 46:24; 1 Nya 7:13 Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni; 49#1 Nya 7:13 wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu. 50Hawa ndio jamaa wa Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia nne.
51 # 1:46; 2:32 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730).
52 # Hes 34:13; Yos 14:1-2 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 53Watu hawa watagawiwa nchi hiyo iwe urithi wao, kulingana na idadi yao ilivyo. 54#Hes 33:54 Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake. 55#Hes 34:13; Yos 11:23; 14:2 Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya makabila ya baba zao, ndivyo watakavyopata urithi. 56Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache.
57 # Mwa 46:11; Kut 6:16; 1 Nya 6:1,16 Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari. 58Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu. 59Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu dada yao. 60#Hes 3:2 Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 61#Law 10:1-2; Hes 3:4; 1 Nya 24:2 Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA. 62#Hes 3:39; 1:49; 18:20-24; 35:2-8; Kum 10:9; 14:27-29; Yos 13:14; 14:3 Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.
63Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko. 64#Hes 1:1; Kum 2:14,15 Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai. 65#Hes 14:26-35; Kum 32:49,50; Zab 90:3-8; Rum 11:22; 1 Kor 10:5; Ebr 3:17,18; Yud 1:5; Hes 14:30; 32:12; Kum 1:36,38; Yos 14:10 Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

Currently Selected:

Hesabu 26: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in