Hesabu 24
24
Aguzi la tatu la Balaamu
1Basi Balaamu alipoona ya kuwa ilimpendeza BWANA kuwabariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, ili kupiga bao, bali alielekeza uso wake jangwani. 2#Hes 11:25; 1 Sam 19:20; 2 Nya 15:1; Mt 7:21-23; 1 Kor 12:8,10 Balaamu akainua macho yake akawaona Israeli wamekaa kabila kwa kabila; Roho ya Mungu ikamjia. 3#Hes 23:7 Akatunga mithali yake, akasema,
Balaamu mwana wa Beori asema,
Yule mtu aliyefumbuliwa macho asema;#24:3 Katika Kiebrania ni ‘aonaye vema’ au ‘aliyefumbwa macho’.
4 #
1 Sam 19:24; Eze 1:28; Dan 8:18; 10:15; 2 Kor 12:2; Ufu 1:10,11 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,
Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,
Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho;
5Mahema yako ni mazuri namna gani, Ee Yakobo,
Maskani zako, Ee Israeli!
6 #
Zab 1:3; Yer 17:8 Mfano wa bonde zimetandwa,
Mfano wa bustani kando ya mto,
Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA,
Mfano wa mierezi kando ya maji.
7 #
1 Sam 15:32; 2 Sam 5:12; 1 Fal 4:21; 1 Nya 14:2; Isa 2:2; 9:7 Maji yatatiririka kutoka ndoo zake,#24:7 au ‘maji yatabubujika kutoka ndoo zake’.
Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi.
Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi,
Na ufalme wake utatukuzwa.
8Mungu amemleta kutoka Misri,
Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati;
Atawameza mataifa walio adui zake,
Ataivunja mifupa yao vipande vipande.
Atawachoma kwa mishale yake.
9 #
Mwa 12:3; 49:9; 27:29; Kut 23:23; Zab 122:6; Mt 25:40,45 Aliinama, akalala mfano wa simba,
Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha?
Na abarikiwe kila akubarikiye,
Na alaaniwe kila akulaaniye.
10Hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu akayapiga makofi; Balaki akamwambia Balaamu, Nilikuita ili unilaanie adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa mara tatu hizi. 11Basi sasa kimbilia mahali pako; niliazimu kukuheshimu sana; lakini, tazama, BWANA amekuzuilia heshima.
12Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionitumia, nikisema, 13Hata Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.
14Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho.
Aguzi la nne la Balaamu
15Akatunga mithali yake akasema,
Balaamu mwana wa Beori asema,
Yule mtu aliyefumbwa macho asema,
16Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,
Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu.#24:16 Au ‘Mungu mkuu’.
Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,
Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,
17 #
Ayu 19:25-27; Zek 12:10; Yud 1:14; Ufu 1:7; Yer 23:5; Dan 2:14; Lk 1:32,33; Ebr 1:8; Ufu 22:16; Mwa 49:10; Zab 110:2 Namwona, lakini si sasa;
Namtazama, lakini si karibu;
Nyota itatokea katika Yakobo
Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli;
Nayo itazipigapiga pembe za Moabu,#24:17 Au ‘vipaji vya nyuso za Moabu’.
Na kuwavunjavunja wana wote wa ghasia.#24:17 Au vichwa vya wazawa wa Sethi.
18 #
Mwa 27:37; 2 Sam 8:14; Zab 60:8-12; Isa 34:5; 63:1; Amo 9:12 Na Edomu itakuwa milki
Seiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake;
Israeli watakapotenda kwa ushujaa.
19Mwenye kutawala atakuja kutoka Yakobo,
Atawaangamiza watakaobaki mjini.
20Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema,
Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa;
Lakini mwisho wake atapata uharibifu.
21Kisha akamwangalia Mkeni, akatunga mithali yake, akasema,
Makao yako yana nguvu,
Na kiota chako kimewekwa katika jabali.
22Pamoja na haya Wakeni wataangamizwa,
Hadi Ashuru atakapokuchukua mateka.
23Akatunga mithali yake akasema,
Ole wao! Ni nani atakayepona, Mungu atakapofanya haya?
24 #
Mwa 10:4; Isa 23:1; Dan 11:30; Mwa 11:14; Law 26:28; Kum 28:36; Mt 23:37 Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu,
Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha,
Yeye naye atapata uharibifu.
25Basi Balaamu akainuka, akaondoka na kurudi mahali pake; Balaki naye akaenda zake.
Currently Selected:
Hesabu 24: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.