YouVersion Logo
Search Icon

Hesabu 1

1
Hesabu ya kwanza ya Waisraeli
1 # Hes 26:1-51; Kut 19:1; Law 27:34; Hes 10:12; Kut 25:22; Law 1:1 BWANA akanena na Musa katika jangwa la Sinai, hemani mwa kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kutoka kwao nchi ya Misri, akamwambia, 2#Kut 30:12; 38:26; Hes 26:2-4,63,64; 1 Nya 21:2; 2 Sam 24:2 Fanyeni hesabu ya watu wote wa Israeli, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mwanamume mmoja mmoja; 3kuanzia aliye na umri wa miaka ishirini na zaidi, wote wawezao kutoka kwenda vitani katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kufuata majeshi yao. 4#Hes 2:2; 1 Nya 27:1 Tena mwanamume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha nyumba ya baba zake. 5#Mwa 29:32; Kut 1:2; Kum 33:6; Ufu 7:4 Haya ndiyo majina ya wanaume watakaokusaidia; Wa Reubeni; Elisuri mwana wa Shedeuri. 6Wa Simeoni; Shelumieli mwana wa Suri-shadai. 7#Hes 7:12; 10:14; Rut 4:20; 1 Nya 2:10; Lk 3:32 Wa Yuda; Nashoni mwana wa Aminadabu. 8Wa Isakari; Nethaneli mwana wa Suari. 9Wa Zabuloni; Eliabu mwana wa Heloni. 10Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri. 11Wa Benyamini Abidani mwana wa Gideoni. 12Wa Dani; Ahiezeri mwana wa Amishadai. 13Wa Asheri; Pagieli mwana wa Okirani. 14#Hes 2:14 Wa Gadi; Eliasafu mwana wa Deueli. 15Wa Naftali; Ahira mwana wa Enani. 16#Mwa 6:4; Kut 18:21; Hes 7:2; 1 Nya 5:24; Amu 6:15; Kut 18:21; Kum 1:15 Hao ndio waliochaguliwa na mkutano, wakuu wa makabila ya baba zao; nao ndio vichwa vya wa wale maelfu ya Israeli. 17Basi Musa na Haruni wakawatwaa watu hao, wanaume waliotajwa majina yao; 18#Ezr 2:59; Neh 7:61; Ebr 7:3 nao waliwakutanisha watu wote, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, nao wakaonesha ukoo wa vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, kwa nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, mmoja mmoja. 19#Hes 26:1,2; 1 Nya 27:23,24; 2 Sam 24:1 Kama BWANA alivyomwagiza Musa, ndivyo alivyowahesabu huko katika jangwa la Sinai.
20Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanamume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi wote walioweza kwenda vitani; 21wale waliohesabiwa katika kabila la Reubeni, walikuwa watu elfu arubaini na sita na mia tano (46,500) mmoja mmoja.
22 # 2 Sam 22:35; Zab 44:3; 60:12; 1 Kor 16:13; 2 Kor 3:5; Efe 6:12 Katika wana wa Simeoni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, wale waliohesabiwa kama hesabu ya majina, kichwa kwa kichwa, kila mwanaume kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 23wale waliohesabiwa katika kabila la Simeoni, walikuwa watu elfu hamsini na tisa na mia tatu (59,300).
24 # Mwa 30:11; 49:19; Yos 4:12; Ufu 7:5 Katika wana wa Gadi, kwa kufuata vizazi vyao, jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 25wale waliohesabiwa katika kabila la Gadi, walikuwa watu elfu arubaini na tano, mia sita na hamsini (45,650).
26 # Mwa 29:35; 49:8-10; Zab 78:68; Mt 1:2; Ebr 7:14; Ufu 5:5 Katika wana wa Yuda, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 27wale waliohesabiwa katika kabila la Yuda, walikuwa watu elfu sabini na nne na mia sita (74,600).
28Katika wana wa Isakari, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kwa hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 29wale waliohesabiwa katika kabila la Isakari, walikuwa watu elfu hamsini na nne na mia nne (54,400).
30Katika wana wa Zabuloni, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 31wale waliohesabiwa katika kabila la Zabuloni, walikuwa watu elfu hamsini na saba na mia nne (57,400).
32 # Mwa 30:24; 48:15,20; Zab 60:7; 78:67; Yer 7:15 Katika wana wa Yusufu, maana katika wana wa Efraimu, vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani, 33wale waliohesabiwa katika kabila la Efraimu, walikuwa watu elfu arubaini na mia tano (40,500).
34Katika wana wa Manase, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 35wale waliohesabiwa katika kabila la Manase, walikuwa watu elfu thelathini na mbili na mia mbili (32,200). 36#Mwa 35:16-18; 44:20; 49:27; Zab 68:27; Ufu 7:8 Katika wana wa Benyamini, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 37wale waliohesabiwa katika kabila la Benyamini, walikuwa watu elfu thelathini na tano na mia nne (35,400).
38 # Mwa 30:5,6; 49:16,17 Katika wana wa Dani, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 39wale waliohesabiwa katika kabila la Dani, walikuwa watu elfu sitini na mbili na mia saba (62,700).
40Katika wana wa Asheri, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 41wale waliohesabiwa katika kabila la Asheri, walikuwa watu elfu arubaini na moja na mia tano (41,500).
42Katika wana wa Naftali, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani; 43wale waliohesabiwa katika kabila la Naftali, walikuwa watu elfu hamsini na tatu na mia nne (53,400).
44 # Hes 26:64 Hao ndio waliohesabiwa, ambao Musa na Haruni na wale wakuu wa Israeli watu kumi na wawili waliwahesabu; walikuwa kila mmoja kwa ajili ya nyumba ya baba zake. 45Basi hao wote waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa kufuata nyumba za baba zao kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi; wote walioweza kwenda vitani katika Israeli; 46#Mwa 13:16; Kut 12:37; 38:26; Kum 10:22; Hes 26:51; 1 Fal 4:20 hao wote waliohesabiwa walikuwa ni wanaume elfu mia sita na tatu, mia tano na hamsini (603,550).
47 # Hes 2:33; 3:1; 26:57; 1 Nya 6:1; 21:6 Lakini Walawi kwa kulifuata kabila la baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao. 48Kwa kuwa BWANA alinena na Musa, na kumwambia, 49#Hes 26:62 Hilo kabila la Lawi tu usilihesabu, wala usiitie hesabu yao katika wana wa Israeli; 50#Kut 31:18; 32:26; Hes 3:7,8,23; 4:15-33 lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi,#1:50 Kut 25:16: Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa. na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote; wao wataichukua hiyo maskani, na vyombo vyake vyote; nao wataitumikia, na kupanga hema zao kwa kuizunguka maskani pande zote. 51#Hes 10:17,21 Tena hapo maskani itakapokwenda mbele, Walawi wataishusha; tena hapo maskani itakaposimamishwa, Walawi wataisimamisha; na mgeni atakayekaribia atauawa. 52Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika kambi yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo bendera yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo. 53#Law 10:6; Hes 8:19; 16:46; 1 Sam 6:19; Hes 8:24; 1 Nya 23:32; 2 Nya 13:10 Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wahudumu katika hiyo Hema Takatifu. 54Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.

Currently Selected:

Hesabu 1: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in