Nehemia 2
2
Nehemia aenda Yuda
1 #
Ezr 7:1
Ikawa katika mwezi wa Nisani,#2:1 Mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiyahudi. mwaka wa ishirini wa mfalme Artashasta, na divai imewekwa mbele yake, nikaishika ile divai, nikampa mfalme. Nami mpaka sasa sikuwa na huzuni mbele ya mfalme wakati wowote. 2#Mit 15:13 Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana. 3#1 Fal 1:31; Dan 2:4; 5:10; Neh 1:3; Zab 137:5 Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto? 4#1 Sam 1:13; Mit 3:6 Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. 5Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unitume mpaka Yuda, niende katika mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. 6#Neh 5:14 Mfalme akaniuliza, (malkia akiwa ameketi karibu naye), Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Nawe utarudi lini? Hivyo mfalme akaona vema kunituma; nami nikampa muda. 7Tena nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na nipewe nyaraka kwa watawala walio ng'ambo ya Mto, ili wanikubalie kupita hadi nifike Yuda; 8#Ezr 10:6,9; Neh 3:7; Ezr 5:5; Mit 21:1; Isa 66:14; Dan 1:9; Mdo 7:10 nipewe na waraka kwa Asafu, mwenye kuutunza msitu wa mfalme, ili anipe miti ya kutengenezea boriti kwa malango ya ngome ya hekalu, na kwa ukuta wa mji; na kwa nyumba ile nitakapoishi mimi. Naye mfalme akanipa, maana mkono mwema wa Mungu wangu ulikuwa juu yangu.
9Ndipo nikafika kwa watawala wa mkoa walio ng'ambo ya Mto, nikawapa nyaraka hizo za mfalme. Naye mfalme alikuwa ametuma maofisa wa jeshi lake na wapanda farasi pamoja nami. 10Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli.
Nehemia akagua kuta za Yerusalemu
11 #
Ezr 8:32
Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu. 12Kisha nikaondoka usiku, mimi pamoja na watu wachache; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe. 13#2 Nya 26:9; Neh 3:13; 1:3; Yer 5:10 Nikatoka nje usiku, kwa njia ya lango la bondeni, nikashika njia iendayo kwenye kisima cha joka, na lango la jaa; nikazitazama kuta za Yerusalemu, zilizokuwa zimebomoka; na malango yake yameteketezwa kwa moto. 14#2 Fal 20:20; 2 Nya 32:30; Neh 3:15 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama niliyemganda. 15#2 Sam 15:23; Yer 31:40; Yn 18:1 Kisha nikapanda usiku kando ya kijito, nikautazama ukuta; kisha nikarudi nyuma, nikaingia kwa lango la bondeni, nikarejea hivyo. 16Wala maofisa hawakujua nilikokwenda, wala niliyotenda; tena nilikuwa sijawaambia Wayahudi, makuhani, wakuu, maofisa, wala watu wengine waliokuwa wakiifanya kazi hiyo.
Uamuzi wa kuzijenga kuta
17 #
1 Sam 11:2; Neh 1:3; Zab 44:13; Yer 24:9; Omb 3:45,46; Eze 5:14 Kisha nikawaambia, Mnaona hali hii dhaifu tuliyo nayo, jinsi Yerusalemu ulivyo hali ya ukiwa, na malango yake yalivyoteketezwa kwa moto; haya! Na tuujenge tena ukuta wa Yerusalemu, ili tusiwe shutumu tena. 18#2 Sam 2:7 Nikawaeleza habari ya mkono wa Mungu wangu ulivyokuwa mwema juu yangu; pia na maneno ya mfalme aliyoniambia. Nao wakasema, Haya! Na tuondoke tukajenge. Basi wakaitia mikono yao nguvu kwa kazi hiyo njema. 19#Zab 44:13; 79:4 Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme? 20#Zab 127:1; Rum 8:31; Ezr 4:3; Yn 4:9; Mdo 8:21 Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.
Currently Selected:
Nehemia 2: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.