Nahumu UTANGULIZI
UTANGULIZI
Nahumu mkazi wa mji wa Elkoshi, alitoa ujumbe wa hukumu kwa mji wa Ninawi, makao makuu ya Ashuru. Kama maana ya jina, yaani “faraja” au “mfariji” lilivyo ndivyo amekuwa mtoa ujumbe wa faraja nyingi kwa watu wa Yuda.
Karne ya nane Kabla ya Kristo kuzaliwa, taifa la Ashuru lilipata nguvu nyingi, lilipanua himaya yake kwa kuteka mataifa madogo ya Palestina. Yuda walitozwa ushuru na kodi kubwa. Baada ya miaka kama mia moja Ashuru lilipungua nguvu, Babeli iliinuka kijeshi na kimamlaka. Adui wa Ashuru walifurahi. Yuda alitegemea hukumu ya Mungu kutolewa kwa taifa jeuri na katili (3:19).
Ujumbe wa Nahumu umewekwa kwa njia ya mashairi kwamba Mungu wa haki ataadhibu wenye ukatili na udhalimu na wote wapingao matakwa yake (1:11-15; 2:1). Wenye maisha yasiyo adili nao wataadhibiwa. Ninawi utaadhibiwa kwa kuwa umedhulumu Yuda (1:12-13) na mataifa mengine (3:1-7). Yuda itaokolewa (1:2). Unabii wa Nahumu ulitimia mwaka 612 Kabla ya Kristo Kuzaliwa, Ninawi ulipotekwa na Wababeli.
Yaliyomo:
1. Mamlaka ya Mungu, Sura 1
2. Maangamizi kwa Ninawi, Sura 2
3. Dhambi ya Ninawi, Sura 3
Currently Selected:
Nahumu UTANGULIZI: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.