YouVersion Logo
Search Icon

Mambo ya Walawi 22

22
Matumizi ya sadaka takatifu
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 2#Hes 6:3; 15:31; Kut 13:12; 28:38; Hes 18:32; Kum 15:19 Nena na Haruni na wanawe, ili washughulikie kwa uangalifu vitu vitakatifu vya wana wa Israeli ambavyo wanitakasia mimi, tena wasilinajisi jina langu takatifu; mimi ndimi BWANA. 3#Law 7:20 Waambie, Mtu yeyote wa kizazi chenu chote katika vizazi vyenu, atakayevikaribia vile vitu vitakatifu, ambavyo wana wa Israeli wamtakasia BWANA, naye ana unajisi, mtu huyo atatengwa asiwe mbele zangu; mimi ndimi BWANA. 4#Law 15:2,13; Hes 19:11,22 Mtu yeyote wa kizazi cha Haruni aliye na ukoma, au kisonono; asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu yeyote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka; 5#Law 11:24; 15:7,19 au mtu amgusaye mnyama atambaaye, wa kumpatia unajisi, au kwamba amgusa mtu wa kumpatia unajisi, kwa unajisi wowote ule alio nao; 6#Ebr 10:22 huyo mtu atakayegusa kitu chochote namna hiyo atakuwa najisi hata jioni, naye hatakula katika vitu vitakatifu, asipooga mwili wake majini. 7#Hes 18:11 Jua likiisha kuchwa atakuwa safi; kisha baadaye atakula katika vitu vitakatifu, maana ni chakula chake. 8#Kut 22:31; Law 17:15; Eze 44:31 Nyamafu au mnyama aliyeraruliwa na wanyama asile, asijitie unajisi kwa hiyo nyama; mimi ndimi BWANA. 9#Kut 28:43; Hes 18:22 Basi kwa hiyo watayashika maagizo yangu, wasije wakachukua dhambi kwa hayo, nao wakafa humo, wakiyanajisi; mimi ndimi BWANA niwatakasaye. 10#Kut 29:33; Hes 3:10; 1 Sam 21:6 Mgeni yeyote asile katika kitu kitakatifu; mgeni wa kuhani akaaye kwake, au mtumishi aliyeajiriwa, asile katika kitu kitakatifu. 11Lakini kuhani akinunua mtu yeyote kwa fedha zake, yeye atakula katika hicho; na hao waliozaliwa nyumbani mwake watakula katika chakula chake. 12Na binti ya kuhani ikiwa ameolewa na mgeni, asile katika sadaka ya kuinuliwa katika vitu vile vitakatifu. 13#Mwa 38:11; Hes 18:11 Lakini ikiwa binti ya kuhani ni mjane, au ameachwa na mumewe, wala hana mtoto, kisha amerudi na kuishi katika nyumba ya baba yake, kama vile katika ujana wake, yeye atakula katika chakula cha baba yake; lakini mgeni yeyote asile katika chakula hicho. 14#Law 5:15,16 Tena kama mtu yeyote akila katika kitu kilicho kitakatifu pasipo kukijua, ndipo ataongeza sehemu ya tano juu ya kitu hicho, na kumpa kuhani kitu hicho kitakatifu. 15#Hes 18:32 Wala wasivinajisi vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, wavisongezavyo kwa BWANA; 16hata wakawatwika ule uovu uletao hatia, hapo walapo vitu vyao vitakatifu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.
Sadaka zinazokubalika
17Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 18#Hes 15:14 Nena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote, uwaambie, Mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni mojawapo ya nadhiri zao, au kama ni sadaka yoyote ya hiari, watakayomtolea BWANA kuwa sadaka ya kuteketezwa; 19ili mpate kukubaliwa, mtaleta dume mkamilifu, katika ng'ombe, au katika kondoo, au katika mbuzi. 20#Kum 17:1; 15:21; Mal 1:8,14; Efe 5:27; Ebr 9:14; 1 Pet 1:19 Lakini mnyama yeyote aliye na kilema msimtoe; kwa kuwa hatakubaliwa kwa ajili yenu. 21#Hes 15:3,8; Kum 23:21; Zab 61:8; 65:1; Mhu 5:4,5 Na mtu yeyote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng'ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema chochote ndani yake. 22Kipofu, au aliyevunjika mahali, au kiwete au aliye na vidonda, au aliye na upele, au aliye na upele, hamtamtolea BWANA wanyama hao, wala msiwasongeze kwa BWANA kwa njia ya moto juu ya madhabahu. 23#Law 21:18 Ng'ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa. 24Mnyama aliyeumia mapumbu yake, au kusetwa, au kuvunjwa, au kukatwa, msimtolee BWANA; wala msifanye hivi katika nchi yenu. 25#Hes 15:15; Mal 1:14 Wala msisongeze chakula cha Mungu wenu katika wanyama hao mmojawapo kitokacho mkononi mwa mgeni; kwa sababu uharibifu wao uko ndani yao, wana kilema ndani yao; hawatakubaliwa kwa ajili yenu.
26Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia, 27#Kut 22:30 Hapo ng'ombe, kondoo au mbuzi, akizaliwa, atakuwa pamoja na mamaye muda wa siku saba; na siku ya nane na baadaye atakubaliwa kuwa ni sadaka ya kutolewa kwa BWANA kwa njia ya moto. 28#Kum 22:6 Tena kama ni ng'ombe, au kondoo, msimchinje huyo na mwanawe, wote wawili kwa siku moja. 29#Zab 107:22; 116:17; Amo 4:5 Tena mtakapomchinjia BWANA dhabihu ya shukrani, mtamchinja ili mpate kukubaliwa. 30Italiwa siku iyo hiyo; msisaze kitu chake hata asubuhi; mimi ndimi BWANA. 31#Law 19:37; Hes 15:40; Kum 4:40 Kwa hiyo mtayashika maagizo yangu, na kuyafanya; mimi ndimi BWANA. 32#Isa 6:3; Mt 6:9; Lk 11:2; Yn 12:28 Wala msilinajisi jina langu takatifu; lakini nitatakaswa mimi katika wana wa Israeli; mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi, 33#Kut 6:7 niliyewaleta mtoke nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu; mimi ndimi BWANA.

Currently Selected:

Mambo ya Walawi 22: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy