Yoshua 4
4
Mawe kumi na mawili yasimamishwa pale Gilgali
1 #
Kum 27:2; Yos 3:17 Ikawa, hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo BWANA akanena na Yoshua, akamwambia, 2#Hes 13:2; 34:18; Kum 1:23; Yos 1:4-15; 3:12; 1 Fal 18:31 Haya, twaeni watu wanaume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja, 3kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende na mawe hayo, mkayaweke mahali pale kambini ambapo mtalala usiku huu. 4Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa ameteua tangu hapo awali, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja; 5naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya makabila ya wana wa Israeli; 6#Kut 12:26; 13:14; Kum 6:20; Zab 44:1; 78:3-6; Isa 38:16 ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya? 7#Yos 3:13; Kut 12:14; Hes 16:40; 1 Kor 11:24 Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yaliondoka mbele ya sanduku la Agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalisimama; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele. 8Basi wana wa Israeli walifanya vile vile kama Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, kama BWANA alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya makabila ya wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayarundika huko. 9#Mwa 28:18; Yos 24:27; 1 Sam 7:12 Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la Agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo. 10Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hadi mambo yote BWANA aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka. 11Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la BWANA likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu. 12#Hes 32:20 Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila la Manase, wakavuka, wakiwa wamebeba silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia; 13walikuwa kama watu elfu arubaini waliobeba silaha tayari kwa vita, waliovuka mbele ya BWANA, waende vitani, hadi nchi tambarare za Yeriko. 14#Yos 3:7; 1 Sam 2:30; 1 Nya 29:12,25; 2 Nya 1:1; 32:23 Siku ile BWANA alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake.
15Kisha BWANA akanena na Yoshua, akamwambia, 16#Kut 25:16; Ufu 11:19; Yos 3:15 Haya, uwaamuru makuhani, hao waliolichukua sanduku la ushuhuda, kwamba wakwee juu kutoka mle katika Yordani. 17Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani. 18Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la Agano la BWANA walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kufurika katika kingo zake zote, kama yalivyokuwa hapo kwanza.
19 #
Yos 5:9; 15:7; 1 Sam 11:14,15; Amo 4:4; 5:5; Mik 6:5 Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko. 20Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali. 21Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini? 22Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu. 23#Kut 14:21; Neh 9:11; Zab 77:16,19; 78:13; Isa 43:16; 63:12 Kwa sababu BWANA, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hadi mlipokwisha kuvuka kama BWANA, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka; 24#Kut 9:16; Kum 28:10; 1 Sam 17:46; 1 Fal 8:42; 2 Fal 5:15; 19:19; Zab 89:7; 106:8; Yer 32:40; Dan 3:26-29; Kut 15:16; 1 Nya 29:12; Kut 14:31; Kum 6:2; Zab 76:6-8; Yer 10:7 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, na ili nanyi mpate kumcha BWANA, Mungu wenu, milele.
Currently Selected:
Yoshua 4: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.