YouVersion Logo
Search Icon

Yeremia 13

13
Kitani cha kiunoni
1BWANA akaniambia hivi, Nenda ukajinunulie kitambaa cha kitani, ukajifunge kiunoni, wala usikitie majini. 2Basi nikanunua kitambaa cha kitani sawasawa na neno la BWANA, nikajivika viunoni. 3Nalo neno la BWANA likanijia mara ya pili, kusema, 4#Zab 137:1; Mik 4:10 Twaa kitambaa kile ulichonunua, kilicho viunoni mwako, kisha ondoka, nenda mpaka mto Frati, ukaufiche huko katika pango la jabali. 5Basi nikaenda, nikakificha karibu na mto Frati, kama BWANA alivyoniamuru. 6Hata ikawa, baada ya siku nyingi, BWANA akaniambia, Ondoka, nenda mpaka mto Frati, ukakitwae kile kitambaa, nilichokuamuru kukificha huko. 7#Isa 64:6; Yer 24:8; Omb 3:45 Ndipo nikaenda mpaka mto Frati, nikachimba, nikakitwaa kile kitambaa katika mahali pale nilipokificha; na tazama, kitambaa kilikuwa kimeharibika, hakikufaa tena kwa lolote. 8Ndipo neno la BWANA likanijia, kusema, 9#Law 26:19 BWANA asema hivi, Jinsi iyo hiyo nitakiharibu kiburi cha Yuda, na kiburi kikuu cha Yerusalemu. 10#2 Nya 36:15,16; Yer 9:14; 11:8 Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyo yao, na kufuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, watakuwa hali moja na kitambaa hiki kisichofaa kwa lolote. 11#Mwa 17:7; Kut 19:5; Yer 33:9 Maana kama vile mshipi unavyoshikamana na kiuno cha mtu, ndivyo nilivyowashikamanisha nami nyumba yote ya Israeli; na nyumba yote ya Yuda, asema BWANA; wapate kuwa watu kwangu mimi, na jina, na sifa, na utukufu; lakini hawakutaka kusikia.
Ishara ya chupa ya mvinyo
12Basi utawaambia neno hili, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kila chupa itajazwa divai; nao watakuambia, Je, sisi hatujui ya kuwa kila chupa itajazwa divai? 13#Zab 60:3; Isa 63:6; Yer 25:27; Eze 23:32-34; Ufu 14:10 Ndipo utakapowaambia, BWANA asema hivi, Tazama, nitawajaza ulevi wenyeji wote wa nchi hii, hata wafalme wanaoketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu. 14Nitawagonganisha, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; sitahurumia, wala sitaachilia, wala sitarehemu, hata nisiwaangamize.
Tishio la kupelekwa uhamishoni
15 # Kum 32:29 Sikilizeni ninyi, kategeni masikio yenu; msifanye kiburi; maana BWANA amenena. 16#Yos 7:19; 1 Sam 6:5; Yoe 2:12; Amo 8:9; Isa 5:30; 59:9; Zab 44:19 Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene. 17Bali kama hamtaki kusikia, roho yangu italia kwa siri, kwa sababu ya kiburi chenu; na jicho langu litalia sana na kutoka machozi mengi, kwa kuwa kundi la BWANA limechukuliwa mateka.
18 # 2 Fal 24:12 Mwambie mfalme, na mama ya mfalme,
Nyenyekeeni na kuketi chini;
Kwa maana vilemba vyenu vimeshuka,
naam, taji la utukufu wenu.
19 # Law 26:31 Miji ya Negebu imefungwa malango yake,
wala hapana mtu wa kuyafungua;
Yuda amechukuliwa mateka;
amechukuliwa kabisa mateka.
20 # Yer 6:22 Inua macho yako, Ee Yerusalemu, ukawatazame hawa wanaokuja kutoka kaskazini; liko wapi kundi lako ulilopewa, kundi lile zuri? 21Utasema nini wewe, atakapowaweka rafiki zako kuwa kichwa juu yako, ikiwa wewe mwenyewe umewafundisha kuwa juu yako? Je! Huzuni haitakushika, kama uchungu wa mwanamke aliye katika kuzaa? 22#Yer 16:10; Isa 47:2; Nah 3:5 Nawe ukisema moyoni mwako, Mbona mambo haya yamenipata mimi? Ni kwa sababu ya wingi wa uovu wako, marinda yako yamefunuliwa, na visigino vya miguu yako vimeumia. 23Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoadoa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya. 24Kwa sababu hiyo nitawatawanya, kama makapi yapitayo, kwa upepo wa jangwani. 25#Ayu 20:29; Yer 10:14; Mik 3:11 Hiyo ndiyo kura yako, fungu lako ulilopimiwa na mimi, asema BWANA; kwa kuwa umenisahau, na kuutumainia uongo. 26#Omb 1:8; Hos 2:10 Kwa ajili ya hayo, mimi nami nitayafunua marinda yako mbele ya uso wako, na aibu yako itaonekana. 27#Yer 5:8; 2:20; Isa 65:7 Nimeona machukizo yako, naam, uzinifu wako, na ubembe wako, na uasherati wa ukahaba wako, juu ya milima katika mashamba. Ole wako, Ee Yerusalemu! Hutaki kutakaswa; mambo hayo yataendelea hata lini?

Currently Selected:

Yeremia 13: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in