YouVersion Logo
Search Icon

Isaya 25

25
Sifa kwa kukombolewa katika udhalimu
1 # Kut 15:2; Hes 23:19 Ee BWANA, wewe u Mungu wangu;
Nitakutukuza na kulihimidi jina lako;
Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu,
Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.
2 # Yer 51:37 Kwa sababu umefanya mji kuwa ni rundo;
Mji wenye boma kuwa ni magofu;
Jumba la wageni kuwa si mji;
Hautajengwa tena milele.
3 # Ufu 11:13 Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza,
Miji ya mataifa yatishayo itakuogopa.
4 # Zab 46:1-11; Nah 1:7 Maana umekuwa ngome ya maskini,
Ngome ya mhitaji katika dhiki yake,
Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani,
Na kivuli wakati wa joto;
Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa,
Kama dhoruba ipigayo ukuta.
5Kama vile joto katika mahali pakavu
Utaushusha mshindo wa wageni;
Kama ilivyo joto kwa kivuli cha wingu,
Wimbo wa hao watishao utashushwa.
6 # Mit 9:2; Mt 22:4; Dan 7:14; Mt 8:11 Na katika mlima huu BWANA wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. 7#2 Kor 3:15; Efe 1:17 Naye katika mlima huu atauharibu utando uliowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. 8#Isa 26:19; Hos 13:14; 2 Kor 5:4; Ebr 2:14; Mwa 49:18; Tit 2:13; 1 Kor 15:54; Ufu 7:17; 21:4 Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.
9Katika siku hiyo watasema,
Tazama, huyu ndiye Mungu wetu,
Ndiye tuliyemngoja atusaidie;
Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja,
Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
10 # Isa 15:1—16:14; Yer 48:1-47; Eze 25:8-11; Amo 2:1-3; Sef 2:8-11 Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji machafu. 11#Ayu 40:11,12; Isa 2:10-12,15-17 Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake. 12#Isa 26:5 Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hadi mavumbini.

Currently Selected:

Isaya 25: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in