YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 9

9
Baa la tano: Ugonjwa juu ya wanyama wafugwao
1 # Kut 8:1; Yer 22:1 Ndipo BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, yuasema, Wape ruhusa watu wangu ili waende wanitumikie. 2#Kut 8:2; Rum 2:5 Kwani ukikataa kuwapa ruhusa waende, na kuzidi kuwazuia, 3#Kut 7:4; 1 Sam 6:3,5; Ayu 27:11; Zab 39:10; Lk 11:20; Mdo 13:11 tazama, mkono wa BWANA uko juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng'ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana. 4#Kut 8:22 Kisha BWANA atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu chochote cha wana wa Israeli. 5Naye BWANA akaweka muda, akasema, Kesho BWANA atalifanya jambo hili katika nchi. 6#Zab 78:50 BWANA akalifanya jambo hilo siku ya pili, na wanyama wote wa kufugwa wa Misri wakafa; lakini katika wanyama wa wana wa Israeli hakufa hata mmoja. 7#Kut 8:32 Farao akatuma watu, na tazama, hapana mmoja aliyekufa katika wanyama wa wana wa Israeli. Lakini moyo wa Farao ulikuwa mzito, wala hakuwapa hao watu ruhusa waende zao.
Baa la sita: Majipu
8BWANA akawaambia Musa na Haruni, Jitwalieni konzi za majivu ya tanuri, kisha Musa ayarushe juu kuelekea mbinguni mbele ya Farao. 9#Ufu 16:2 Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri, nayo yatakuwa majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama, katika nchi yote ya Misri. 10#Ufu 16:2 Basi wakatwaa majivu ya tanuri, na kusimama mbele ya Farao; na Musa akayarusha juu mbinguni nayo yakawa ni majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama. 11#2 Tim 3:9 Nao wale waganga hawakuweza kusimama mbele ya Musa kwa sababu ya hayo majipu, kwa maana hao waganga walikuwa na majipu, na Wamisri wote walikuwa nayo. 12#Kut 4:21; 7:14; 8:32; 10:1,20; 14:8; Kum 2:30; Yos 11:20; Isa 63:17; Yn 12:40; Rum 9:18; Yak 1:13-16; Kut 4:21 BWANA akaufanya mgumu moyo wa Farao, asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyomwambia Musa.
Baa la saba: Mvua yenye radi na barafu
13 # Kut 8:20 BWANA akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa waende ili wanitumikie. 14#Kum 3:24; 33:26; 2 Sam 7:22; 1 Nya 17:20; Zab 71:19; 86:8; Isa 45:5-25; Yer 10:6,7 Kwani wakati huu nitaleta mapigo yangu yote juu ya moyo wako, na juu ya watumishi wako, na juu ya watu wako; ili upate kujua ya kuwa hapana mmoja mfano wa mimi ulimwenguni kote. 15#Kut 3:20 Kwa kuwa wakati huu ningekwisha kuunyosha mkono wangu, na kukupiga wewe na watu wako, kwa tauni, nawe ungekatiliwa mbali na kuondolewa katika nchi; 16#Rum 9:17; Mit 16:4; 1 Pet 2:9 lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote. 17Nawe, je! Hata sasa wajitukuza juu ya watu wangu, usiwape ruhusa waende zao? 18Tazama, kesho wakati kama huu, nitanyesha mvua ya mawe nzito sana, ambayo mfano wake haujakuwa huko Misri tangu siku ile ilipoanza kuwa hata hivi sasa. 19Basi sasa tuma watu wahimize kuingiza ndani mifugo yako na hayo yote uliyo nayo mashambani; kwani kila mtu na kila mnyama apatikanaye mashambani, wasioletwa nyumbani, hiyo mvua ya mawe itanyesha juu yao, nao watakufa. 20Yeye aliyelicha neno la BWANA miongoni mwa watumishi wa Farao aliwakimbiza watumishi wake na wanyama wake waingie nyumbani; 21na yeye asiyelitia moyoni neno la BWANA akawaacha watumishi wake na wanyama wake mashambani.
22 # Ufu 16:21 BWANA akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, ili iwe mvua ya mawe katika nchi yote ya Misri, juu ya wanadamu na juu ya wanyama, na juu ya mboga zote za mashamba, katika nchi yote ya Misri. 23#Yos 10:11; Zab 18:13; 78:47; Isa 30:30; Eze 38:22; Ufu 8:7 Musa akaunyosha mkono wake kuelekea mbinguni; na BWANA akaleta ngurumo na mvua ya mawe, na moto ukashuka juu ya nchi; BWANA akanyesha mvua ya mawe juu ya nchi yote ya Misri. 24#Ufu 8:7; 16:21 Basi palikuwa na mvua ya mawe, na moto uliochanganyikana na ile mvua ya mawe, nzito sana, ambayo mfano wake haukuwapo katika nchi yote ya Misri tangu ilipoanza kuwa taifa. 25#Zab 105:33 Na ile mvua ya mawe ikapiga kila kilichokuwako mashambani, binadamu na mnyama, katika nchi yote ya Misri; hiyo mvua ya mawe ikapiga kila mmea wa mashambani, na kuuvunja kila mti wa mashamba. 26#Kut 9:4,6; 11:7; Isa 32:18,19 Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe. 27#Kut 10:16; 2 Nya 12:6; Zab 129:4; Dan 9:14 Farao akatuma watu, na kuwaita Musa na Haruni, na kuwaambia, Mimi nimekosa wakati huu; BWANA ni mwenye haki, na mimi na watu wangu tu waovu. 28#Kut 8:8,28; 10:17; Mdo 8:24 Mwombeni BWANA; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi. 29#1 Fal 8:22,38; Zab 143:6; Isa 1:15; Zab 24:1; 1 Kor 10:26 Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia BWANA mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya BWANA. 30#Isa 26:10 Lakini, wewe na watumishi wako, najua ya kuwa ninyi hamtamcha BWANA Mungu bado. 31#Rut 1:22; 2:23 Kitani na shayiri zilipigwa; maana shayiri zilikuwa na masuke na kitani zilikuwa katika kutoa maua. 32Lakini ngano na kusemethi hazikupigwa; maana, zilikuwa hazijakua bado. 33#Kut 8:12 Musa akatoka mjini, kutoka kwa Farao, akamwinulia BWANA mikono yake; na zile ngurumo na ile mvua ya mawe zikakoma, wala mvua haikunyesha juu ya nchi. 34Farao alipoona ya kwamba mvua na mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akazidi kufanya dhambi, na kuufanya moyo wake mzito, yeye na watumishi wake. 35Moyo wa Farao ukawa ni mgumu naye hakuwapa wana wa Israeli ruhusa waende zao; kama BWANA alivyonena kwa kinywa cha Musa.

Currently Selected:

Kutoka 9: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in