Kutoka 7
7
1 #
Kut 4:16; Yer 1:10 BWANA akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako. 2Utanena hayo yote nikuagizayo; na ndugu yako Haruni atanena na Farao, ili awape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake. 3#Mdo 7:36; Kut 4:7; 11:9 Nami nitaufanya mgumu moyo wa Farao, nami nitazifanya kuwa nyingi ishara zangu na ajabu zangu katika nchi ya Misri. 4#Kut 6:6; 10:1 Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri, na kuyatoa majeshi yangu, watu wangu, hao wana wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa hukumu zilizo kuu. 5#Kut 8:22; 14:4,18; Zab 9:16; 59:13; Kut 3:20 Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, hapo nitakapounyosha mkono wangu juu ya Misri na kuwatoa wana wa Israeli watoke kati yao. 6Musa na Haruni wakafanya vivyo hivyo; kama BWANA alivyowaambia, ndivyo walivyofanya. 7#Kum 29:5; 31:2; 34:7; Mdo 7:23,30 Huyo Musa alikuwa ni mtu wa miaka themanini umri wake, na Haruni alikuwa ni mtu wa miaka themanini na mitatu, hapo waliponena na Farao.
Fimbo ya miujiza ya Haruni
8BWANA akanena na Musa na Haruni, akawaambia, 9#Isa 7:11; Yn 2:18; 6:30; Kut 4:2,17 Farao atakaponena nanyi, na kuwaambia, Jifanyieni miujiza; ndipo utakapomwambia Haruni, Shika fimbo yako, uibwage chini mbele ya Farao, ili iwe nyoka. 10#Kut 4:3 Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya vivyo hivyo kama BWANA alivyowaambia; Haruni akaibwaga fimbo yake chini mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. 11#Mwa 41:8; Dan 2:2; 2 Tim 3:8; Kut 7:22; 8:7,18; 2 Kor 11:13; 2 The 2:9,11; 2 Tim 3:13; 2 Pet 2:13; Ufu 12:9; 13:14 Ndipo Farao naye akawaita wajuzi na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo hivyo kwa uganga wao. 12Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao. 13#Kut 4:21 Moyo wa Farao ukawa ni mgumu asiwasikize; kama BWANA alivyonena.
MABAA KUMI
Baa la kwanza: Maji yageuka damu
14 #
Kut 8:15; 10:20,27 BWANA akamwambia Musa, Moyo wa Farao ni mzito, anakataa kuwapa watu ruhusa waende zao. 15#Kut 4:2,3 Mwendee Farao asubuhi; tazama, atoka kwenda majini; nawe simama karibu na ufuo wa mto ili upate kuonana naye; na ile fimbo iliyogeuzwa kuwa nyoka utaichukua mkononi mwako. 16#Kut 3:12,18; 5:1,3 Nawe umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, amenituma nije kwako, kusema, Wape watu wangu ruhusa, ili wapate kunitumikia jangwani; nawe, tazama! Hujasikia hata sasa. 17#Ufu 16:4,6; Zab 9:16; Eze 20:48; 25:17; Yoe 3:17; Kut 4:9 BWANA asema, Katika jambo hili utanijua ya kuwa mimi ndimi BWANA; tazama, nitayapiga haya maji yaliyo mtoni kwa fimbo hii niliyo nayo mkononi mwangu, nayo yatageuzwa kuwa damu. 18#Kut 7:24 Na hao samaki walio mtoni watakufa, na huo mto utatoa uvundo; nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni. 19#Kut 8:5; 9:22; 10:12 BWANA akamwambia Musa, Mwambie Haruni, Shika fimbo yako, kaunyoshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya mito yao, juu ya vijito vyao, na juu ya maziwa ya maji yao, na juu ya visima vyao vyote vya maji, ili yageuke kuwa damu, nako kutakuwa na damu katika nchi yote ya Misri, katika vyombo vya mti, na katika vyombo vya jiwe. 20#Kut 17:5; Zab 78:44; 105:29 Musa na Haruni wakafanya hivyo, kama BWANA alivyowaambia; naye akaiinua ile fimbo, na kuyapiga maji yaliyokuwa mtoni, mbele ya Farao, mbele ya watumishi wake; na hayo maji yote yaliyokuwa katika mto yakageuzwa kuwa damu. 21Hao samaki waliokuwa mtoni nao wakafa; na ule mto ukatoa uvundo, Wamisri wasipate kunywa maji ya mtoni; na ile damu ilikuwa katika nchi yote ya Misri. 22Lakini waganga wa Misri wakafanya mfano wa hayo kwa uganga wao; na moyo wake Farao ukawa mgumu, wala hakuwasikiza, kama BWANA alivyonena. 23#Mit 29:1 Farao akazunguka na kuingia nyumbani mwake, wala hata hilo hakuliweka moyoni. 24Wamisri wote wakachimbachimba kando ya mto ili wapate maji ya kunywa; maana, hawakuweza kuyanywa yale maji ya mtoni. 25Zikatimia siku saba, baada ya BWANA kuupiga ule mto.
Currently Selected:
Kutoka 7: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.