YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 6

6
Ukombozi wa Waisraeli wahakikishwa
1 # Kut 11:1; 12:31 BWANA akamwambia Musa, Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusa kwenda zao, na kwa mkono hodari atawafukuza katika nchi yake.
2 # Mwa 17:1; 28:3; 35:11; Kut 3:13-15 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni BWANA; 3#Zab 68:4; Yn 8:58; Ufu 1:4 nami nilimtokea Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi,#6:3 Katika Kiebrania ni ‘EL-SHADDAI’ ‘Mungu Mwenyezi’ au ‘Mungu mwenye nguvu’. bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao. 4#Mwa 15:18; 17:4,7,8 Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya waliyokaa kama wageni. 5#Kut 2:24 Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu. 6#Kut 3:17; 7:4; 15:13; Kum 26:8; 7:8; Zab 81:6; 136:11; 1 Nya 17:21; Neh 1:10 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni BWANA nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya ukandamizaji wa Wamisri, nami nitawaokoa kutoka utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa; 7#Kum 7:6; 29:13; 2 Sam 7:24; Mwa 17:7,8; Ufu 21:7; Zab 81:6 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwakomboaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri. 8#Mwa 15:18; 26:3 Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo niliinua mkono wangu, niwape Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA. 9Musa akawaambia wana wa Israeli maneno haya; lakini hawakumsikiliza Musa kwa ajili ya uchungu wa moyo, na kwa ajili ya utumwa mgumu.
10BWANA akasema na Musa, akamwambia, 11Ingia ndani, ukaseme na Farao, mfalme wa Misri, ili awape ruhusa wana wa Israeli watoke nchi yake. 12#Yer 1:6 Musa akanena mbele za BWANA, akasema, Tazama, hao wana wa Israeli hawakunisikiza mimi; basi huyo Farao atanisikizaje, mimi niliye na midomo isiyo tohara?#6:12 ‘Mimi niliye na kigugumizi au asiye na ufasaha wa kuhutubia’. 13BWANA akanena na Musa na Haruni, akawaagiza wawaendee wana wa Israeli, na Farao, mfalme wa Misri, ili awatoe hao wana wa Israeli katika nchi ya Misri.
Nasaba ya Musa na Haruni
14 # Mwa 49:9; 1 Nya 5:3 Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni. 15#Mwa 46:10; 1 Nya 4:24 Na wana wa Simeoni; ni Yemueli, na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli mwana wa mwanamke wa Kikanaani; hao ni jamaa za Simeoni. 16#Hes 3:17-20; 26:57-58; 1 Nya 6:16-19; Mwa 46:11; 1 Nya 6:1 Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni,#6:16 Pengine huitwa ‘Gershomu’ Tafsiri yake ni ‘mkimbizi’ tazama Kut 2:22. na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba. 17Wana wa Gershoni; ni Libni, na Shimei, kulingana na jamaa zao. 18#Hes 26:57; 1 Nya 6:18 Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.
19Na wana wa Merari; ni Mali, na Mushi. Hizi ni jamaa za hao Walawi kulingana na vizazi vyao. 20#Kut 2:1,2; Hes 26:59 Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba. 21#Hes 16:1; 1 Nya 6:37,38 Na wana wa Ishari; ni Kora, na Nefegi, na Zikri. 22#Law 10:4; Hes 3:30 Na wana wa Uzieli; ni Mishaeli, na Elisafani, na Sithri. 23#Rut 4:19,20; 1 Nya 2:10; Mt 1:4; Law 10:1; Hes 3:2 Haruni akamwoa Elisheba, binti ya Aminadabu, dada yake Nashoni; naye akamzalia Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. 24#Hes 26:11 Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora. 25#Hes 25:7,11,12; Yos 24:33 Na Eleazari mwana wa Haruni akamwoa mmoja miongoni mwa binti za Putieli; naye akamzalia Finehasi. Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba wa Walawi kulingana na jamaa zao. 26#Kut 7:4; 12:17; Hes 33:1 Hawa ni Haruni yeye yule, na Musa yeye yule, BWANA aliowaambia, akisema, Watoeni wana wa Israeli watoke nchi ya Misri sawasawa na majeshi yao. 27#Kut 32:7; 33:1; Zab 77:20 Ni hao walionena na Farao mfalme wa Misri ili wawatoe wana wa Israeli watoke Misri; hao ni Musa yeye yule, na Haruni yeye yule.
Musa na Haruni watii amri za Mungu
28Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri, 29#Kut 7:2 BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA; mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo. 30#Kut 4:10; Yer 1:6 Musa akanena mbele ya BWANA, Mimi ni mtu mwenye midomo isiyo tohara, Farao atanisikizaje?

Currently Selected:

Kutoka 6: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in