YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 26

26
Hema ya kukutania
1 # Kut 25:9; 29:42,43; 40:2,17; Mdo 7:44,45; Ebr 8:2-5; 9:2-11; Ufu 21:3; 1 Kor 12:28; Efe 4:11,12; Ebr 1:14 Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi. 2Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; mapazia yote yatakuwa ya kipimo kimoja. 3#1 Kor 12:4-12 Mapazia matano yataungwa pamoja, hili na hili; na mapazia matano mengine yataungwa pamoja, hili na hili. 4#Efe 4:13; Kol 2:2,19 Kisha utafanya tanzi za rangi ya samawati upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake, vivyo hivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyo, katika fungu la pili. 5Fanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upande wa mwisho wa ile pazia iliyo katika kuungana kwa pili; hizo tanzi zitaelekeana. 6Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganisha hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo; na hiyo maskani itakuwa ni moja.
7 # Kut 36:14 Nawe fanya mapazia ya singa za mbuzi yawe hema juu ya maskani; fanya mapazia kumi na moja. 8Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne; hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja. 9Kisha utaunganisha mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalikunja hapo upande wa mbele wa ile hema. 10Fanya tanzi hamsini upande wa mwisho wa pazia lile lililo la mwisho katika hayo yaliyounganywa pamoja, na tanzi hamsini upande wa mwisho wa lile pazia lililo nje katika hayo ya pili yaliyounganywa pamoja. 11Tena ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja. 12Na kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, ile nusu ya pazia iliyosalia, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani. 13Na hiyo dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili, ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika. 14#Kut 36:19; Hes 24:5 Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.
Muundo wa hema la kukutania
15Nawe fanya hizo mbao za maskani za mti wa mjohoro, zenye kusimama. 16Kila ubao utakuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wake kila ubao utakuwa dhiraa moja na nusu. 17Kila ubao utakuwa na ndimi mbili, zenye kuunganishwa huu na huu; ndivyo utakavyozifanya mbao zote za maskani. 18Kisha ufanye zile mbao za maskani, mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini. 19#Kut 38:27 Nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile mbao ishirini, vitako viwili chini ya ubao mmoja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya ubao mwingine kupokea zile ndimi zake mbili; 20na upande wa pili wa maskani, upande wa kaskazini, mbao ishirini; 21na vitako vyake vya fedha arubaini; vitako viwili chini ya ubao mmoja, na vitako viwili chini ya ubao mwingine. 22Kisha ufanye mbao sita kwa ajili ya upande wa nyuma wa maskani kuelekea magharibi. 23Tena ufanye mbao mbili kwa ajili ya hizo pembe za maskani zilizo upande wa nyuma. 24Upande wa chini zitakuwa ni mbili mbili; vivyo hivyo zitaunganishwa pamoja mbao pacha hata ncha ya juu katika pete ya kwanza; zote mbili ndivyo zitakavyokuwa; zitakuwa kwa ajili ya hizo pembe mbili. 25Mbao zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha, vitako kumi na sita; vitako viwili chini ya ubao mmoja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili. 26#Kut 36:31; Rum 15:1; Gal 6:2 Nawe fanya mataruma ya mti wa mshita; mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani, 27na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi. 28Na hilo taruma la katikati, lililo katikati ya zile mbao litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu. 29Na hizo mbao utazifunika dhahabu, na pete zake za kutilia yale mataruma utazifanya za dhahabu; na hayo mataruma utayafunika dhahabu. 30#Kut 25:9,40; 27:8; Mdo 7:44; Ebr 8:5 Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake uliooneshwa mlimani.
Pazia
31 # Law 16:2; 2 Nya 3:14; Mt 27:51; Mk 15:38; Lk 23:45; Ebr 9:3 Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi; 32kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne. 33#Ebr 6:19; 9:3-5; Kut 25:16; 40:21; Yos 4:11; 1 Sam 4:6; 6:19; 1 Fal 8:6; 1 Nya 15:1; Ufu 11:19; Law 16:2; Mt 24:15 Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana. 34#Kut 25:21; 40:20; Law 16:2; Ebr 9:5 Nawe utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. 35#Kut 40:22-24; Ebr 9:2 Na ile meza utaiweka nje ya pazia, na kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini; na ile meza utaiweka upande wa kaskazini.
36 # Kut 36:37 Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa Hema, cha nyuzi za rangi ya buluu, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji wa taraza. 37#Kut 36:38 Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu; nawe utasubu vitako vya shaba vitano kwa ajili yake.

Currently Selected:

Kutoka 26: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in