YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 22

22
Sheria za malipizo
1 # 2 Sam 12:6; Lk 19:8; Mit 6:31 Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja. 2#Kut 20:15; Law 19:11; Kum 5:19; Mt 6:19; 24:43; Lk 18:20; Rum 13:9; Efe 4:28; 1 Pet 4:15; Hes 35:27 Mwizi akipatikana akiwa yu hali ya kuvunja mahali, naye akapigwa hata akafa, hapatakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake. 3#Kut 21:2; Mt 18:25 Lakini kama jua limekucha juu yake, ndipo patakuwa na malipizo ya damu kwa ajili yake; ingempasa kutoa malipo kamili; akiwa hana kitu, na auzwe kwa ajili ya wizi wake. 4#Kut 21:16; Mit 6:31 Kama hicho kitu kilichoibwa chapatikana hai mkononi mwake, kama ni ng'ombe, au punda, au kondoo; atalipa thamani yake mara mbili.
5Mtu akilisha mifugo kama shamba, au shamba la mizabibu, akimwacha mnyama wake, akala katika shamba la mtu mwingine; atalipa katika vitu vilivyo vizuri vya shamba lake mwenyewe, au vya mizabibu yake.
6Ukiwaka moto, na kushika penye miiba, na ngano zilizofungwa miganda, au ngano ambazo hazijakatwa, au shamba, likateketea; yeye aliyeuwasha huo moto lazima atalipa.
7Mtu akimpa mwenziwe amana ya fedha au vitu vingine amtunzie, na vitu vile vikaibwa katika nyumba ya mtu huyo; mwizi akipatikana, atalipa thamani yake mara mbili. 8Mwizi asipopatikana, ndipo mwenye nyumba atakaribia mbele ya Mungu, ionekane kwamba si yeye aliyetia mkono na kutwaa vyombo vya mwenziwe. 9#Kum 25:1; 2 Nya 19:10 Kila jambo la kukosana, kama ni la ng'ombe, au la punda, au la kondoo, au la mavazi, au la kitu chochote kilichopotea, ambacho mtu mmoja asema ni chake, hilo jambo la watu wote wawili litaletwa mbele ya Mungu; na yeye atakayehukumiwa na Mungu kuwa ni mkosa atamlipa mwenziwe thamani yake mara mbili.
10Mtu akimpa mwenziwe punda, au ng'ombe, au kondoo, au mnyama yeyote, ili amtunzie; yule mnyama akafa, au akaumia, au akachukuliwa mtu asione; 11#Ebr 6:16 patakuwa na kiapo cha BWANA katikati ya watu hao wawili, kwamba alipeleka mkono wake kutwaa mali ya mwenziwe, na mwenyewe atakubali hayo, wala hatalipa. 12#Mwa 31:39 Lakini kwamba aliibiwa mnyama huyo, sharti amlipe yule mwenyewe. 13Kama aliraruliwa na mnyama mkali, na amlete uwe ushahidi; hatalipa kwa ajili ya mnyama aliyeraruliwa.
14Mtu akiazima mnyama kwa mwenziwe, naye akaumia huyo mnyama, au akafa, mwenyewe asipokuwapo, lazima atalipa. 15Kama huyo mwenyewe alikuwapo pamoja na mnyama wake, hatalipa; kama ni mnyama wa kukodisha ni gharama ya kukodisha tu atakayepewa mwenyewe.
Sheria za jamii na kidini
16 # Kum 22:28-29 Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe. 17#1 Sam 18:25 Ikiwa baba yake huyo mwanamwali akataa kabisa kumpa, atalipa fedha kama hesabu ya mahari ya mwanamwali ilivyo.
18 # Kum 18:10-11 Usimwache mwanamke mchawi kuishi.
19 # Law 18:23; 20:15-16; Kum 27:21 Mtu yeyote alalaye na mnyama sharti atauawa.
20 # Kum 13:1; 17:2-7; Hes 25:2; Hos 8:14; 1 Fal 18:40 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu yeyote, isipokuwa ni yeye BWANA peke yake, na angamizwe kabisa.
21 # Kut 23:9; Law 19:33-34; 25:35; Kum 10:19; Zek 7:10; Mal 3:5; Kum 24:17-18; 27:19 Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri. 22#Isa 1:17; Eze 22:7; Kum 10:18 Usimtese mjane yeyote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima. 23#Kum 15:9; Ayu 35:9; 34:28; Yak 5:4 Ukiwatesa watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao, 24#Ayu 31:23; Zab 109:9 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.
25 # Law 25:35-38; Kum 15:7-11; 23:19-20; Neh 5:7; Eze 18:8 Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida. 26#Kum 24:10-13; Ayu 24:3; Mit 20:16; Amo 2:8 Ikiwa wewe kwa njia yoyote wapokea nguo ya jirani yako rehani, lazima utamrudishia mbele ya jua kuchwa; 27maana hiyo nguo ni kifuniko chake, hiyo peke yake ni nguo ya ngozi yake; je! Atalalia nini? Itakuwa, hapo atakaponililia mimi, nitasikia; kwa kuwa mimi ni mwenye rehema.
28 # Mdo 23:5; Mhu 10:20; 2 Pet 2:10 Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako. 29#Mit 3:9 Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao wanaume utanipa mimi. 30#Kum 15:19; Law 22:27 Nawe utafanya vivyo hivyo katika ng'ombe wako, na kondoo wako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi. 31#Law 17:15; 19:2; Eze 4:14 Nanyi mtakuwa watu watakatifu kwangu mimi; kwa hiyo msiile nyama yoyote iliyoraruliwa huko kondeni na mnyama wa mwitu; mtawatupia mbwa nyama hiyo.

Currently Selected:

Kutoka 22: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in