YouVersion Logo
Search Icon

Kutoka 11

11
Onyo kabla ya baa la mwisho
1 # Kut 12:31 BWANA akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa. 2#Kut 3:22; 12:35 Basi nena wewe masikioni mwa watu hawa, na kila mwanamume na atake kwa jirani yake, na kila mwanamke atake kwa jirani yake, vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu. 3#Kut 3:21; 12:36; Zab 106:46; 2 Sam 7:9; Est 9:4 BWANA akawapa watu hao kibali machoni pa Wamisri. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake.
4 # Kut 12:12,23,29; Amo 5:17 Musa akasema, BWANA asema hivi, Kama usiku wa manane mimi nitatoka nipite kati ya Misri; 5#Amo 4:10 na wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri watakufa, tangu yule mzaliwa wa kwanza wa Farao aketiye katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa huyo kijakazi aliye pale nyuma ya jiwe la kusagia; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. 6#Amo 5:17 Ndipo kutakuwa na kilio kikuu katika nchi yote ya Misri, ambacho mfano wake haujakuwa bado majira yoyote, wala hautakuwako mfano wake tena kabisa. 7#Yos 10:21; Ayu 5:23; Hos 2:18; Mal 3:18 Lakini katika wana wa Israeli hapana hata mbwa atakayetoa ulimi juu yao, juu ya mtu wala juu ya mnyama; ili kwamba mpate kujua jinsi BWANA anavyowatenga Wamisri na Waisraeli. 8Tena hao watumishi wako wote wataniteremkia kwangu mimi, nao watanisujudia, wakisema, Toka wewe, na hawa watu wote wakufuatao; na baada ya hayo nitatoka. Basi akatoka kwa Farao na hasira kuu.
9BWANA akamwambia Musa, Farao hatawasikiza ninyi; kusudi ajabu zangu ziongezeke katika nchi ya Misri. 10#Kut 9:12; Kum 2:30; Yos 11:20; Isa 63:17; Yn 12:40; Rum 2:5; 9:22 Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.

Currently Selected:

Kutoka 11: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in