YouVersion Logo
Search Icon

2 Samweli 22

22
Wimbo wa Shukrani wa Daudi
1 # Kut 15:1 Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na mkononi mwa Sauli; 2#Mwa 15:1; Kum 32:4; 1 Sam 2:2; Zab 18:2; 91:2; Mit 18:10; Mt 18:11 akasema,
BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,
3 # Ebr 2:13; Mwa 15:1; Zab 3:3; Mit 30:5; Lk 1:69; Mit 18:10; Zab 9:9; 18:2; Isa 32:2; Isa 32:2; Yer 16:19 Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye;
Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na
kimbilio langu;
Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.
4Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa;
Hivyo nitaokoka na adui zangu.
5Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka,
Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
6Kamba za kuzimu zilinizunguka;
Mitego ya mauti ikanikabili.
7 # Zab 116:4; Yon 2:2; Kut 3:7 Katika shida yangu nilimwita BWANA,
Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;
Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,
Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
8 # Amu 5:4; Ayu 26:11; Zab 18:7; 77:18 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka,
Misingi ya mbinguni ikasukasuka
Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
9 # Zab 97:3; Hab 3:5; Ebr 12:29 Kukapanda moshi kutoka puani mwake,
Moto ukatoka kinywani mwake ukala;
Makaa yakawashwa nao.
10 # Isa 64:1 Aliziinamisha mbingu akashuka;
Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.
11 # Zab 104:3 Akapanda juu ya kerubi akaruka;
Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.
12Akafanya giza hema zake za kumzunguka,
Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni.
13Toka mwangaza uliokuwa mbele zake
Makaa ya moto yakawashwa.
14 # Isa 30:30 BWANA alipiga radi toka mbinguni,
Naye Aliye Juu akaitoa sauti yake.
15 # Kum 32:23; Zab 7:13; 77:17; Hab 3:11 Akapiga mishale, akawatawanya;
Umeme, naye akawatimua.
16Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari,
Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa,
Kwa kukemea kwake BWANA,
Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
17Alipeleka kutoka juu, akanishika;
Akanitoa katika maji mengi;
18Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,
Na wale walionichukia;
Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
19Walinikabili siku ya msiba wangu;
Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.
20 # Zab 31:8; 2 Sam 15:26 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi;
Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
21BWANA alinitendea kulingana na haki yangu;
Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa.
22Maana nimezishika njia za BWANA,
Wala sikumwasi Mungu wangu.
23 # Kum 7:12 Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu;
Na kuhusu amri zake, sikuziacha.
24 # Mwa 6:9; Ayu 1:1; Yn 1:47 Nami nilikuwa mkamilifu kwake,
Nikajilinda na uovu wangu.
25Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu;
Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.
26 # Mt 5:7 Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili
Kwa mkamilifu utajionesha kuwa mkamilifu;
27 # Law 26:23 Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu;
Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi.
28 # Kut 3:7; Zab 12:5; Mt 5:3 Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa;
Ila macho yako huwapinga wenye kiburi, uwadhili.
29Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA;
Na BWANA ataniangazia giza langu.
30Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi;
Kwa msaada wa Mungu wangu ninaruka ukuta.
31 # Kum 32:4; Dan 4:37; Ufu 15:3; Zab 12:6; Mit 30:5 Mungu njia yake ni kamilifu;
Ahadi ya BWANA imehakikishwa;
Yeye ndiye ngao yao
Wote wanaomkimbilia.
32 # Kum 32:31; 1 Sam 2:2; Isa 45:5,6 Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA?
Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?
33 # Zab 27:1; Kum 18:13 Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu;
Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.
34 # Hab 3:19 Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu;
Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35Ananifundisha mikono yangu vita;
Hata mikono yangu inaupanda upinde wa shaba.
36Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;
Na unyenyekevu wako umenikuza.
37Umezifanyia nafasi hatua zangu,
Wala miguu yangu haikuteleza.
38Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza;
Wala sikurudi nyuma hadi walipokomeshwa.
39Nami nimewakomesha na kuwapiga wasiweze kusimama;
Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.
40Maana umenijaza nguvu ya kupigana vita;
Ukawafanya adui zangu wafifie chini yangu.
41Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,
Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.
42 # 1 Sam 28:6; Ayu 27:9; Mit 1:28 Walitazama, lakini hapakuwa na wa kuwaokoa;
Walimwita BWANA, lakini hakuwajibu.
43Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi,
Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.
44 # Kum 28:13; Isa 55:5 Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu;
Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa;
Watu nisiowajua watanitumikia.
45Wageni walinijia wakinyenyekea;
Mara tu waliposikia habari zangu,
Walinitii.
46 # Mik 7:17 Wageni nao waliishiwa nguvu,
Wakatoka katika ngome zao wakitetemeka.
47 # Zab 89:26 BWANA yu hai;
Na ahimidiwe mwamba wangu;
Na atukuzwe Mungu wangu, mwamba wa wokovu wangu;
48 # Zab 144:2 Naam, Mungu anilipiziaye kisasi,
Na kuwatweza watu chini yangu,
49Na kuniokoa kutoka kwa adui zangu;
Naam, waniinua juu yao walioniinukia;
Ukaniokoa kutoka kwa watu wajeuri.
50 # Rum 15:9 Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa,
Nami nitaliimbia jina lako.
51Yeye ni mnara wa wokovu#22:51 Au wokovu mkuu. kwa mfalme wake;
Amfanyia fadhili masihi#22:51 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wake,
Kwa Daudi na wazawa wake, hata milele.

Currently Selected:

2 Samweli 22: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in