YouVersion Logo
Search Icon

2 Samweli 15

15
Absalomu anyakua utawala
1 # 2 Sam 12:11; 1 Fal 1:5; Mit 11:2; 16:18 Ikawa baada ya hayo, Absalomu akajiwekea tayari gari na farasi, na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake. 2#Mit 1:16 Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu yeyote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumishi wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli. 3#Mit 12:2 Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza. 4#Amu 9:29 Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au kesi aje kwangu, nimpatie haki yake! 5#Zab 12:2 Tena ikawa hapo alipokaribia mtu yeyote kumsujudia, hunyosha mkono wake, na kumshika, na kumbusu. 6#Rum 16:18 Hivyo ndivyo Absalomu alivyowatendea Israeli wote, waliomwendea mfalme ili wapate hukumu; na hivyo Absalomu akawadanganya watu wa Israeli.
7 # 2 Sam 2:1 Hata ikawa mwisho wa miaka minne, Absalomu akamwambia mfalme, Tafadhali uniache niende nikaondoe nadhiri yangu, niliyomwekea BWANA huko Hebroni. 8#1 Sam 16:2; Mwa 28:20; 1 Sam 1:11; Zab 56:12; 2 Sam 13:38; 14:23,32 Maana mimi mtumishi wako niliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama BWANA akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia BWANA. 9Naye mfalme akamwambia, Nenda kwa amani. Basi akaondoka, akaenda Hebroni.
10Lakini Absalomu akatuma wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anatawala huko Hebroni. 11#1 Sam 9:13; 16:3,5; Mwa 20:5; Mit 14:15; Mt 10:16; Rum 16:18,19 Na watu mia mbili walioalikwa wakatoka Yerusalemu pamoja na Absalomu, wakaenda katika ujinga wao wasijue neno lolote. 12#Zab 41:9; 55:12; Mik 7:5,6; Yos 15:51; Zab 3:1; 43:2 Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Daudi akimbia toka Yerusalemu
13 # Amu 9:3 Mjumbe akamfikia Daudi, akasema, Mioyo ya watu wa Israeli inashikamana na Absalomu. 14#2 Sam 19:9 Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate kwa upesi, na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga. 15Hao watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme, Angalia, sisi watumishi wako tu tayari kutenda lolote atakalolichagua bwana wetu mfalme. 16#2 Sam 12:11; 16:21; 20:3 Basi mfalme akatoka na watu wa nyumbani mwake wote wakafuatana naye. Mfalme akaacha wanawake kumi, masuria, ili kuitunza nyumba. 17Mfalme akatoka, na watu wote wakamfuata; wakakaa kidogo katika Beth-merhaki.#15:17 Kwa maana ya nyumba ya mwisho. 18#2 Sam 8:18 Watumishi wake wote wakapita karibu naye; na Wakerethi wote, na Wapelethi wote, na Wagiti wote, watu mia sita walioandamana naye kutoka Gathi, wakapita mbele ya mfalme.
19 # 2 Sam 18:2 Ndipo mfalme akamwambia Itai, Mgiti, Mbona wewe unakwenda pamoja nasi? Rudi, ukakae na mfalme; maana wewe u mgeni, tena u mtu uliyefukuzwa mahali pako mwenyewe. 20#1 Sam 23:13 Kwa kuwa umekuja jana tu kwa nini nikusumbue leo, na kukuzungusha huku na huko pamoja nasi nami hapa ninaenda niwezapo kwenda? Rudi wewe, ukawarudishe na ndugu zako; rehema na kweli ziwe pamoja nawe. 21#Rut 1:16; 1 Sam 20:3; 2 Fal 2:2-6; Mit 17:17 Naye Itai akamjibu mfalme akasema, Kama aishivyo BWANA, na bwana wangu mfalme aishivyo, hakika yake kila mahali atakapokuwapo mfalme, bwana wangu, ikiwa ni kwa kufa au ikiwa ni kwa kuishi, ndipo atakapokuwapo na mtumishi wako. 22Basi Daudi akamwambia Itai, Haya, nenda ukavuke. Akavuka Itai, Mgiti na watu wake wote, na watoto wadogo wote waliokuwa pamoja naye. 23#1 Fal 2:37; 2 Nya 30:14; Yn 18:1; 2 Sam 16:2; Mt 3:1-3 Na nchi yote ikalia kwa sauti kuu, nao watu wote wakavuka, mfalme mwenyewe naye akavuka kile kijito Kidroni, na hao watu wote wakavuka, wakielekea njia ya nyika.
24 # Hes 4:15 Na tazama, Sadoki naye akaja, na Walawi wote pamoja naye, huku wakilichukua sanduku la Agano la Mungu; kisha wakalitua hilo sanduku la Mungu; Abiathari naye akapanda juu, hadi watu wote walipokwisha kuutoka mji. 25#Zab 43:3; 2 Sam 6:17 Naye mfalme akamwambia Sadoki, Rudisha sanduku la Mungu mjini; nikipata kibali machoni pa BWANA atanirudisha, na kunionesha tena sanduku hili, na maskani yake; 26#Hes 14:8; 2 Sam 22:20; 1 Fal 10:9; 2 Nya 9:8; Isa 62:4; 1 Sam 3:18 lakini akisema kama hivi, Mimi si radhi nawe kabisa; basi, mimi hapa, na anitendee kama aonavyo kuwa vyema. 27#2 Sam 24:11; 1 Sam 9:9 Kisha mfalme akamwambia Sadoki, kuhani, Angalia,#15:27 Au, Je! Wewe si mwonaji? rudini mjini kwa amani, na wana wenu wawili pamoja nanyi, Ahimaasi, mwana wako, na Yonathani, mwana wa Abiathari. 28Angalia, mimi nitangoja penye vivuko vya jangwani, hata litakaponifikia neno la kunipasha habari kutoka kwenu. 29Basi Sadoki na Abiathari wakalichukua sanduku la Mungu, wakalirudisha Yerusalemu; wakakaa huko.
30 # Zek 14:4; Mt 21:1; Lk 19:20; Mdo 1:12; Est 6:12; Isa 20:2; Yer 14:3; Zab 126:6; Mt 5:4; Rum 12:15 Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akapanda huku akilia; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda. 31#Zab 3:1; 55:12; 2 Sam 16:23 Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Hushai anakuwa Mpelelezi wa Daudi
32 # 2 Sam 1:2; 13:9 Ikawa, Daudi alipofika juu, hapo Mungu alipoabudiwa, tazama, Hushai, Mwarki, akaja kumlaki na joho lake likiwa limeraruliwa, tena akiwa na udongo kichwani mwake. 33#2 Sam 19:35 Daudi akamwambia, Ukienda mbele pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu; 34lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu. 35Je! Hawako Sadoki na Abiathari, makuhani, pamoja nawe huko? Basi itakuwa, kila neno utakalolisikia katika jumba la mfalme, utawaambia Sadoki na Abiathari, makuhani. 36Angalia, wanao huko pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani, mwana wa Abiathari; nanyi kwa mikono yao mtanitumia habari ya kila neno mtakalolisikia. 37#2 Sam 16:15,16; 1 Nya 27:33; Mit 17:17 Basi Hushai, rafiki wa Daudi, akaingia ndani ya mji; naye Absalomu akafika akaingia Yerusalemu.

Currently Selected:

2 Samweli 15: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy