YouVersion Logo
Search Icon

2 Samweli 10

10
Kushindwa kwa Waamoni na Washami
1 # 1 Sam 11:1; 2 Sam 17:27; 1 Nya 19:1 Ikawa baadaye, mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe Hanuni, akawa mfalme, badala yake. 2Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahasi, kama babaye alivyonitendea wema mimi. Basi Daudi akatuma kwa mkono wa watumishi wake, ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya Waamoni. 3Lakini wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza? 4#Isa 3:17; 20:4; Yer 13:22,26; Eze 16:37; Mik 1:11; Nah 3:5 Basi Hanuni akawatwaa hao watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawakatia nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao. 5Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wameaibika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi. 6#Mwa 34:30; Kut 5:21; 1 Sam 13:4; 2 Sam 8:3,5 Na Waamoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Waamoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari elfu ishirini, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu moja, na watu wa Tobu watu elfu kumi na mbili. 7#2 Sam 23:8 Naye Daudi aliposikia akamtuma Yoabu, na jeshi lote la mashujaa. 8Waamoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani. 9Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami; 10akawatia nguvu watu waliosalia mkononi mwa Abishai, nduguye, akawapanga juu ya Waamoni. 11Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini Waamoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe. 12#Kum 31:6; 2 Nya 19:11; 1 Sam 4:9; 1 Kor 16:13; 1 Sam 3:18; 2 Sam 15:26; 22:31,32; Zab 20:7; 37:3,5,40; Mit 29:25 Uwe hodari, tuwe na ujasiri, kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye BWANA afanye yaliyo mema machoni pake. 13Basi Yoabu na watu waliokuwa pamoja naye wakakaribia kupigana na Washami; nao wakakimbia mbele yake. 14Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa wana wa Amoni, akaja Yerusalemu.
15Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakakusanyika. 16Naye Hadadezeri akatuma na kuwaleta Washami waliokuwako ng'ambo ya Mto; nao wakaja Helamu, naye Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza. 17Daudi alipoambiwa, akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akaja Helamu. Nao Washami wakajipanga kinyume cha Daudi, wakapigana naye. 18Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi elfu arubaini, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko. 19#Mwa 14:4 Na wafalme wote waliomtumikia Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Israeli, wakawatumikia. Basi Washami wakaogopa kuwasaidia Waamoni tena.

Currently Selected:

2 Samweli 10: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy