YouVersion Logo
Search Icon

2 Wakorintho 3

3
Wahudumu wa Agano Jipya
1 # 2 Kor 5:12; Rum 16:1; Mdo 18:27 Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu? 2#1 Kor 9:2 Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote; 3#Kut 24:12; 31:18; 34:1; Mit 3:3; 7:3; Rum 15:16; Yer 31:33; Eze 11:19; 36:26 mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoiandaa, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.
4Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 5#2 Kor 2:6 Si kwamba tunatosha sisi wenyewe kufikiri kuwa neno lolote ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu unatoka kwa Mungu. 6#Yer 31:31; 1 Kor 11:25; Rum 7:6; Yn 6:63 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. 7#Kut 34:29 Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika; 8#Gal 3:2,5 je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? 9#Kum 27:26; Rum 1:17; 3:21 Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, seuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. 10#Kut 34:29 Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana. 11Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile idumuyo ina utukufu.
12Basi, kwa kuwa mna tumaini la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; 13#Kut 34:33,35 nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; 14#Rum 11:25 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; 15ila hata leo, Torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. 16#Kut 34:34; Rum 11:23,26 Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. 17#Yn 7:39; 8:36; Kut 16:7; 24:17; Rum 8:2 Basi “Bwana” ndiye Roho; lakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 18Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.

Currently Selected:

2 Wakorintho 3: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy