YouVersion Logo
Search Icon

2 Mambo ya Nyakati 6

6
Kuzinduliwa kwa hekalu
1 # 1 Fal 8:12; Kut 20:21; 24:15-18; Law 16:2; Zab 18:8-11; Ebr 12:18 Ndipo Sulemani akanena, BWANA alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. 2Lakini nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele. 3Mfalme akageukia mkutano wote wa Israeli akawabariki, mkutano wote wa Israeli ukiwa umesimama. 4Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema, 5Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu Israeli; 6#2 Nya 12:13; Zab 48:1; 78:68-70; 1 Sam 16:1; 1 Nya 28:4; Zab 89:19,20 lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo; na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli. 7#2 Sam 7:2; 1 Fal 5:3; 1 Nya 17:1; 28:2 Basi ilikuwa moyoni mwake Daudi, baba yangu, kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli. 8#1 Fal 8:18-21; 2 Kor 8:12 Lakini BWANA akamwambia Daudi baba yangu, Kwa kuwa ilikuwa moyoni mwako kujenga nyumba kwa jina langu, ulifanya vema kuwaza hivi moyoni mwako; 9lakini si wewe utakayeijenga nyumba hiyo; ila mwanao atakayetoka katika uzao wako, yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu. 10Basi BWANA amelitimiza neno lile alilolinena; nami nimesimama mahali pa Daudi baba yangu, na kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi, nami nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli. 11#Kut 40:20; 1 Fal 8:9-21; 2 Nya 5:10 Ndimo nilimoliweka hilo sanduku, ambalo ndani yake mna agano la BWANA, alilolifanya na wana wa Israeli.
Sala ya uzinduzi wa hekalu
12 # 1 Fal 8:22; Ezr 9:5; 1 Tim 2:8 Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya BWANA, machoni pa mkutano wote wa Israeli, akainyosha mikono; 13(maana Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano, na kwenda juu kwake dhiraa tatu, na kuisimamisha katikati ya ua; akasimama juu yake, akapiga magoti mbele ya mkutano wote wa Israeli, akaikunjua mikono yake kuelekea mbinguni); 14#Kut 15:11; Kum 4:39; 9:7; 2 Sam 7:22; Zab 86:8; Dan 9:4; Mwa 5:24 akasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa moyo wao wote; 15#1 Nya 22:9,10 uliyemtimizia mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidi; naam, ulinena kwa kinywa chako, ukayatimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo. 16#2 Sam 7:12,16; 1 Fal 2:4; 6:12; 2 Nya 7:18; Zab 132:12 Sasa, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, umtimizie mtumishi wako Daudi, baba yangu, ahadi uliyomwahidia, ukisema, Hutakosa kuwa na mtu machoni pangu, wa kuketi katika kiti cha enzi cha Israeli; wakiwa tu watoto wako wataiangalia njia yao, ili kuiendea torati yangu, kama wewe ulivyokwenda mbele zangu. 17Basi sasa, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, ulithibitishe neno lako, ulilomwambia mtumishi wako Daudi. 18#Zab 113:5,6; 2 Nya 2:6; Isa 66:1; Mdo 7:49 Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga! 19Walakini umwangalie mtumishi wako anayoyaomba, na kusihi, Ee BWANA, Mungu wangu, usikie kilio na maombi anayoyaomba mtumishi wako mbele zako; 20#Zab 33:18; 34:15; Dan 6:10 ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumishi wako, akikabili mahali hapa. 21#Isa 43:25; 44:22 Uyasikie atakayosihi mtumishi wako, na watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa; naam, usikie toka makaoni mwako, toka mbinguni, nawe usikiapo, samehe.
22Ikiwa mtu amemkosea mwenzake, akitiwa kiapo, aapishwe, naye akija na kuapa hapa mbele ya madhabahu yako nyumbani humu; 23#Mit 1:31; Isa 3:11; Rum 2:8 basi, usikie mbinguni, ukatende, ukawahukumu watumishi wako; ukimlipiza mwovu, kumpatilizia njia yake kichwani; ukamfanyie haki mwenye haki, ukimjalia kwa kadiri ya haki yake.
24 # Kum 32:15; Amu 2:11-15; Zab 51:4 Ikiwa watu wako Israeli wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea kwako, na kulikiri jina lako, wakikuomba na kukusihi nyumbani humu; 25basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watu wako Israeli, na kuwarejeza tena katika nchi uliyowapa wao na baba zao.
26 # Law 26:19; 1 Fal 17:1; Lk 4:25 Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, uwatesapo; 27#2 Nya 20:9; 1 Fal 8:35,36; Zab 94:12; Yn 6:45; Zek 10:1 basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumishi wako, na ya watu wako Israeli; uwafundishapo njia njema iwapasayo waiendee; ukainyeshee mvua nchi yako, uliyowapa watu wako iwe urithi.
28 # 2 Nya 20:9 Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukame, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao, au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote; 29yoyote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii; 30#1 Nya 28:9; Zab 11:4 basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe umjuaye moyo; (maana wewe peke yako ndiwe uijuaye mioyo ya wanadamu); 31ili wakuche wewe, waziendee njia zako, siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.
32 # Kum 4:6-8; Zab 113:3; Isa 56:3-8; Mal 1:11; Yn 10:16; 12:20; Mdo 8:27 Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; 33basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.
34Ikiwa watu wako wametoka kupigana na adui zao, utakakowatuma kokote, wakikuomba kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 35basi uyasikie huko mbinguni wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao. 36#Ayu 15:14-16; Mit 20:9; Mhu 7:20; Yak 3:2; 1 Yoh 1:8 Wakikukosa, (maana hakuna mtu asiyekosa), hata uwakasirikie, na kuwatia mikononi mwa adui zao, wawahamishe, na kuwachukua mateka mpaka nchi iliyo mbali au iliyo karibu; 37#Yer 24:6,7 basi wakikumbuka katika nchi walikohamishwa, na kutubu, na kukusihi katika nchi ya uhamisho wao, wakisema, Tumekosa, tumetenda kwa ukaidi, tumefanya maovu; 38#Yer 29:12,13 wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; 39basi uyasikie toka mbinguni, toka makaoni mwako, wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao; ukawasamehe watu wako, waliokosa juu yako.
40Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa. 41#Zab 132:8-16; 1 Nya 28:2; Isa 51:10; Neh 9:25 Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema. 42#Zab 89:20-28; Isa 55:3 Ee BWANA, Mungu, usimpe kisogo masihi#6:42 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10). wako; uzikumbuke fadhili za Daudi mtumishi wako.

Currently Selected:

2 Mambo ya Nyakati 6: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in