YouVersion Logo
Search Icon

2 Mambo ya Nyakati 32

32
Uvamizi wa Senakeribu
1 # 2 Fal 18:13; Isa 36:1 Ikawa, baada ya mambo hayo, na uaminifu huo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja, akaingia katika Yuda, akapiga kambi juu ya miji yenye maboma, akadhania kwamba ataipata iwe yake. 2Basi Hezekia, alipoona ya kuwa Senakeribu amekuja, na kuazimia kupigana na Yerusalemu, 3akafanya shauri na wakuu wake, na wakuu wa majeshi yake, kuzuia maji ya chemchemi zilizokuwa nje ya mji; nao wakamsaidia. 4Wakakusanyika watu wengi, wakazizuia chemchemi zote, na kijito kilichopita kati ya nchi, wakisema, Kwa nini, wakifika wafalme wa Ashuru, waone maji mengi? 5#Isa 22:9,10; 2 Nya 25:23; 2 Sam 5:9; 1 Fal 9:24 Hezekia akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele. 6#2 Nya 30:22; Isa 40:2 Akaweka makamanda wa vita juu ya watu, akawakusanya kwake uwandani penye lango la mji, akawatia moyo; akisema, 7#Kum 31:6; Yos 1:6,7; 1 Nya 28:10,20; 2 Nya 20:15; 2 Fal 6:16; Zab 55:18 Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wala msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye; 8#Yer 17:5; 1 Yoh 4:4; Hes 14:9; Kum 20:1,4; 31:6,8; 2 Nya 13:12; Zab 18:2; 46:7,11; Mit 18:10; Isa 41:10-14; Amo 5:14; Rum 8:31 kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo BWANA, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
9 # 2 Fal 18:17 Na baada ya hayo Senakeribu mfalme wa Ashuru, akatuma watumishi wake waende Yerusalemu, (naye alikuwapo mbele ya Lakishi, na uwezo wake wote pamoja naye,) kwa Hezekia, mfalme wa Yuda, na kwa Yuda wote waliokuwako Yerusalemu, kusema, 10Senakeribu, mfalme wa Ashuru, asema hivi, Mwatumainia nini hata mkae mkihusuriwa katika Yerusalemu? 11Siye Hezekia anayewashawishi, mtolewe kufa kwa njaa na kwa kiu, akisema, BWANA, Mungu wetu, atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru? 12Si yeye Hezekia huyo aliyeondoa mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaamuru Yuda na Yerusalemu, akisema, Abuduni mbele ya madhabahu moja, na juu yake mtafukiza uvumba? 13#2 Fal 18:33-35; Zab 115:4-8 Je! Ninyi hamjui mimi na baba zangu tuliyowafanyia watu wote wa nchi? Je! Miungu ya mataifa wa nchi iliweza kuokoa kwa lolote nchi zao na mkono wangu? 14Ni yupi miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, ndipo Mungu wenu aweze kuwaokoa ninyi na mkono wangu? 15#Kut 5:2; Dan 3:15; Yn 19:10,11 Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lolote, wala wa ufalme wowote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu? 16Na watumishi wake wakazidi kusema juu ya BWANA Mungu, na juu ya Hezekia, mtumishi wake.
17 # 2 Fal 19:9 Tena akaandika waraka, kumtukana BWANA, Mungu wa Israeli, na kumwambia, akisema, Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono wangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu. 18#2 Fal 18:28 Wakawalilia kwa sauti kuu, kwa lugha ya Kiyahudi, watu wa Yerusalemu waliokuwako ukutani ili kuwaogofya, na kuwafadhaisha; ndipo wapate kuutwaa mji. 19#Isa 10:10; Kum 4:28; 2 Fal 19:18; Zab 115:4; 135:15-18; Yer 1:16; 10:3; Hos 8:5,6 Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu, kana kwamba kuitaja miungu ya mataifa wa nchi, iliyo kazi ya mikono ya watu.
Kushindwa na kufa kwa Senakeribu
20Na kwa ajili ya hayo Hezekia mfalme, na Isaya nabii, mwana wa Amozi, wakaomba, wakalia hata mbinguni. 21Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatia mbali wapiganaji vita wote, na majemadari, na makamanda, kambini mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake kwa aibu. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga. 22#Zab 18:48-50; Isa 31:5 Ndivyo BWANA alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote. 23#2 Nya 17:5; 1 Nya 29:25; 2 Nya 1:1 Watu wengi walimletea BWANA zawadi huko Yerusalemu, na vitu vya thamani kwa Hezekia, mfalme wa Yuda; hata yeye akatukuka tangu wakati ule machoni pa mataifa yote.
Ugonjwa wa Hezekia
24 # Isa 38:1 Katika siku hizo Hezekia akaugua akawa katika hatari ya kufa; akamwomba BWANA; naye akasema naye, akampa ishara. 25#Kum 32:6; Zab 116:12; Hos 14:2; Lk 17:17; Kum 8:12-17; 2 Fal 14:10; 2 Nya 25:19; Hab 2:4; 1 Tim 3:6; 1 Pet 5:5,6; 2 Nya 24:18 Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. 26#Yer 26:18; 2 Fal 20:19 Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya BWANA siku za Hezekia.
Ustawi na ufanisi wa Hezekia
27Naye Hezekia akawa na mali nyingi mno na heshima; akajitengenezea hazina za fedha, za dhahabu, za vito, za manukato, za ngao, na za namna zote za vyombo vya thamani; 28ghala pia za mazao ya nafaka na mvinyo na mafuta; na malisho ya mifugo ya namna zote, na makundi mazizini. 29#2 Nya 29:12 Tena akajitengenezea miji, na mali za kondoo na ng'ombe kwa wingi; maana Mungu alimtajirisha sana sana. 30#Isa 22:9 Naye huyo Hezekia ndiye aliyezuia chemchemi ya juu ya maji ya Gihoni, akayaleta chini moja kwa moja upande wa magharibi wa mji wa Daudi. Akafanikiwa Hezekia katika kazi zake zote. 31#Isa 39:1; Mwa 22:1; Kum 8:2; Yn 1:12 Lakini kuhusu wajumbe wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuuliza ajabu iliyofanywa katika nchi, Mungu akamwacha, ili amjaribu, ili kwamba ayajue yote yaliyokuwamo moyoni mwake. 32#Isa 36:1; 2 Fal 18:1 Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na matendo yake mema, tazama, yameandikwa katika maono ya nabii Isaya, mwana wa Amozi, katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli. 33#1 Sam 2:30; Mit 10:7 Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.

Currently Selected:

2 Mambo ya Nyakati 32: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in