2 Mambo ya Nyakati 3
3
Sulemani ajenga hekalu
1 #
1 Fal 6:1; 1 Nya 29:19; Yn 2:19-21; 1 Kor 6:19; Mwa 22:2; 1 Nya 22:1 Ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya BWANA huko Yerusalemu, juu ya mlima Moria, pale BWANA alipomtokea Daudi babaye alipotengeza mahali pale alipoagiza Daudi, katika kiwanja cha kupuria cha Arauna#3:1 Au, Ornani. Myebusi. 2Akaanza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. 3#1 Fal 6:2 Basi hivi ndivyo vipimo#3:3 Neno ‘vipimo’ katika lugha ya Kiebrania ni ‘misingi’. vya majengo ya nyumba ya Mungu alivyoviweka Sulemani. Urefu wake ulikuwa dhiraa sitini na upana wake dhiraa#3:3 Dhiraa tazama Kutoka 25:10. ishirini. 4#1 Fal 6:3 Na ukumbi uliokuwa mbele yake, urefu wake ulikuwa sawa na upana wa nyumba ulikuwa dhiraa ishirini, na kimo chake mia moja na ishirini; akaufunikiza ndani kwa dhahabu safi. 5#1 Fal 6:17 Nayo nyumba kubwa ilizungushiwa miti ya miberoshi, aliyoifunikiza kwa dhahabu safi, juu yake akaichora mitende na minyororo. 6Akaipamba nyumba kwa vito iwe na uzuri; nayo dhahabu ilikuwa dhahabu ya Parvaimu. 7Tena, akaifunikiza kwa dhahabu nyumba, na boriti, na vizingiti, na kuta zake, na milango yake; akachora makerubi kutani. 8Akaifanya nyumba ya patakatifu pa patakatifu; urefu wake sawa na upana wa nyumba, ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa ishirini; akaifunikiza kwa dhahabu safi, ya talanta mia sita. 9Na uzani wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Alivifunika vyumba vyake ghorofani kwa dhahabu. 10#1 Fal 6:23 Na ndani ya nyumba ya patakatifu pa patakatifu akatengeneza makerubi mawili ya kuchonga; wakayafunika kwa dhahabu. 11Na mabawa ya makerubi hayo urefu wake ulikuwa mikono ishirini; bawa moja mikono mitano, likiufikia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la pili. 12Na bawa la kerubi la pili lilikuwa mikono mitano, likiufikia ukuta wa nyumba; na bawa la pili mikono mitano, likishikana na bawa la kerubi la kwanza. 13Yakaenea mabawa ya makerubi hayo dhiraa ishirini; yakasimama juu ya miguu yao, na nyuso zao ziliielekea nyumba. 14#Kut 26:31; Mt 27:51; Ebr 9:3 Akalifanya pazia la samawati na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaitengeneza makerubi. 15#1 Fal 7:15; Yer 52:21 Tena akafanya mbele ya nyumba nguzo mbili za mikono thelathini na tano kwenda juu kwake, na mataji yaliyokuwa juu yake moja moja ilikuwa mikono mitano. 16Akafanya minyororo ndani ya chumba cha ndani, akaiweka juu ya vichwa vya nguzo; akafanya makomamanga mia moja, akayaweka juu ya hiyo minyororo. 17Akazisimamisha nguzo hizo mbele ya hekalu, moja upande wa kulia, na ya pili upande wa kushoto; akaliita jina la ile ya kulia Yakini,#3:17 Yakini: maana yake imedhaniwa kuwa ‘atathibitisha.’ na jina la ile ya kushoto Boazi.#3:17 Boazi maana yake imedhaniwa kuwa Imo nguvu.
Currently Selected:
2 Mambo ya Nyakati 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.