YouVersion Logo
Search Icon

2 Mambo ya Nyakati 10

10
Uasi juu ya Rehoboamu
1 # 1 Fal 12:11 Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme. 2#1 Fal 11:40 Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia tendo hilo (maana alikuwa Misri, alikokwenda alipomkimbia mfalme Sulemani) Yeroboamu akarudi kutoka Misri. 3Wakatuma ujumbe, wakamwita, Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 4#1 Sam 8:11-18; 1 Fal 4:7; 5:15; 9:15; Mt 11:29,30; 23:4; 1 Yoh 5:3 Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako, na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia. 5Akawaambia, Mnirudie baada ya siku tatu. Watu wakaenda zao. 6#Ayu 8:8,9; 32:7 Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mnanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa? 7#1 Fal 12:7; Neh 5:19; Zab 112:5; Mit 15:1 Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, hapo watakuwa watumishi wako siku zote.
8 # 2 Sam 17:14; 2 Nya 25:16; Mit 1:25; 13:20; Mhu 10:2 Lakini akaliacha shauri lile la wazee walilompa, akataka shauri kwa wale vijana wa rika yake, waliokuwa washauri wake. 9Akawaambia, Je! Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakisema, kongwa alilotutwika baba yako utufanyie liwe jepesi. 10Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliosema nawe, wakinena, Baba yako alilifanya kongwa letu kuwa zito, lakini wewe tufanyie jepesi; uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 11Basi kama baba yangu aliwatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge.
12Basi Yeroboamu na watu wote wakamjia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 13#Mit 12:13; 14:16 Mfalme akawajibu kwa ukali; mfalme Rehoboamu akaliacha shauri la wazee, akasema nao kwa shauri la vijana, 14akinena, Baba yangu aliwafanyia kongwa zito, nami nitawaongezea; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, lakini mimi nitawapiga kwa nge. 15#Mwa 50:20; 1 Sam 2:25; 1 Fal 12:15,24; Amo 3:6; 1 Fal 11:29 Basi mfalme hakuwasikia watu wale; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni. 16Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hawasikilizi, watu wakamjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; kila mtu aende zake hemani, enyi Israeli, sasa itunze nyumba yako mwenyewe ewe Daudi. Basi wakaenda zao Israeli wote hemani kwao. 17Lakini kuhusu wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu alitawala juu yao. 18Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakampiga kwa mawe hadi akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu. 19#1 Fal 12:19; 2 Fal 17:21-23; 2 Nya 13:5-7; Mhu 2:19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo.

Currently Selected:

2 Mambo ya Nyakati 10: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in