YouVersion Logo
Search Icon

1 Samweli 6

6
Sanduku la Agano larudishwa Israeli
1Basi, hilo sanduku la BWANA lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi saba. 2#Mwa 41:8; Kut 7:11; Dan 2:2; 5:7; Mt 2:4 Nao Wafilisti wakawaita makuhani na waaguzi, wakasema, Tulifanyieje sanduku la BWANA? Tuonesheni jinsi tuwezavyo kulirudisha mahali pake. 3#Kut 23:15; Kum 16:16; Law 5:15; 6:6 Nao wakajibu, Mkilirudisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe kitupu; lakini msikose kumpelekea na matoleo ya kosa; hivyo mtapona, tena mtafunuliwa ni kwa sababu gani mkono wake haukuondolewa kwenu. 4#Yos 13:3; Amu 3:3 Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa tutakayompelekea, yatakuwa ya namna gani? Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya wakuu wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya wakuu wenu. 5#1 Sam 5:6; Yos 7:19; 1 Nya 16:28; Isa 42:12; Yer 13:16; Mal 2:2; Yn 9:24; Ufu 14:7; 16:9; Kut 9:3; 1 Sam 5:6,11; Zab 39:10; Mdo 13:11 Kwa hiyo mtafanya sanamu za majipu yenu, na sanamu za panya wenu wanaoiharibu nchi; nanyi mtamtukuza huyo Mungu wa Israeli; huenda ataupunguza uzito wa mkono wake juu yenu, na juu ya miungu yenu, na juu ya nchi yenu. 6#Kut 7:13; 8:15; 3:19,20; 6:1; Zab 105:38 Mbona, basi, mnaifanya mioyo yenu migumu, kama vile wale Wamisri, na yule Farao, walivyoifanya mioyo yao migumu? Hata na hao, baada ya kuwadhihaki, je! Hawakuwaruhusu watu waende, nao wakaondoka? 7#2 Sam 6:3; Hes 19:2 Basi sasa jifanyieni gari jipya, mtwae na ng'ombe wake wawili wakamwao, ambao hawajafungwa nira, nanyi mkawafunge hao ng'ombe garini, na kuwaondoa ndama wao na kuwatia zizini; 8kisha, litwaeni hilo sanduku la BWANA, na kuliweka juu ya gari; na hivyo vitu vya dhahabu, mtakavyompelekea kuwa matoleo ya kosa, mvitie katika kasha kando yake; mkalipeleke sanduku, lipate kwenda.
9 # Yos 15:10 Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni bahati mbaya iliyotupata.
10Basi watu wale walifanya hivyo; wakatwaa ng'ombe wawili wakamuliwao, wakawafunga garini, na ndama wao wakawafunga zizini; 11kisha wakaliweka sanduku la BWANA juu ya gari, pamoja na kasha lenye panya wa dhahabu na sanamu za majipu yao. 12Na hao ng'ombe wakashika njia moja kwa moja kwenda Beth-shemeshi; wakaiandama njia ya barabara, wakaenda wakilia, lakini hawakugeukia upande wa kulia wala wa kushoto; na wakuu wa Wafilisti wakawafuata hata kuufikia mpaka wa Beth-shemeshi. 13Nao watu wa Beth-shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao bondeni; wakainua macho yao, wakaliona sanduku, wakafurahi sana kuliona. 14Na lile gari likaingia katika konde la Yoshua wa Beth-shemeshi, na kusimama pale pale, palipokuwapo jiwe kubwa; basi wakaipasua miti ya lile gari, wakawatoa wale ng'ombe kuwa ni sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. 15Nao Walawi walilishusha sanduku la BWANA, na lile kasha lililokuwa pamoja nalo, lenye vile vitu vya dhahabu; wakaviweka juu ya lile jiwe kubwa; nao watu wa Beth-shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja dhabihu siku iyo hiyo kwa BWANA. 16#Yos 13:3; Amu 3:3; 16:23; 1 Sam 29:2; Sef 2:5 Na hao wakuu watano wa Wafilisti, hapo walipoyaona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo.
17Hii ndiyo hesabu ya yale majipu waliyoyapeleka wale Wafilisti, yawe matoleo ya kosa kwa BWANA; kwa Ashdodi moja, kwa Gaza moja, kwa Ashkeloni moja, kwa Gathi moja, na kwa Ekroni moja; 18na panya wa dhahabu, kwa idadi ya miji yote ya Wafilisti, milki zao wale wakuu watano, miji yenye maboma na vijiji vya mashamba pia. Nalo lile jiwe kubwa, ambalo juu yake waliliweka sanduku la BWANA, liko hata hivi leo hapo kondeni pa Yoshua wa Beth-shemeshi.
Sanduku la Mungu katika Kiriath-yearimu
19 # Kut 19:21; Law 10:1-3; Hes 4:5,15,20; Kum 29:29; 2 Sam 6:7; Kol 2:18; 1 Pet 4:17 Basi BWANA aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-shemeshi, kwa sababu wamechungulia ndani ya hilo sanduku la BWANA, wapata watu sabini, na watu elfu hamsini; nao watu wakalalamika, kwa kuwa BWANA amewapiga watu kwa uuaji mkuu. 20#2 Sam 6:9; Mal 3:2; Ufu 6:17 Nao watu wa Beth-shemeshi wakasema, Ni nani awezaye kusimama mbele za BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Naye atapanda kwenda kwa nani kutoka kwetu? 21#Yos 18:14; Amu 18:12; 1 Nya 13:5,6 Nao wakatuma wajumbe waende kwa wenyeji wa Kiriath-yearimu, kusema, Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; basi shukeni, mkalichukue.

Currently Selected:

1 Samweli 6: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in