1 Wafalme 9
9
Mungu Amtokea Sulemani Tena
1 #
2 Nya 7:11; 1 Fal 7:1; 2 Nya 8:1,6; Mhu 2:4 Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya, 2#1 Fal 3:5; 2 Fal 20:5; Zab 10:17; 34:17; Dan 9:23; 1 Fal 8:29; Kum 11:12 basi, BWANA akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni.
3BWANA akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote; 4#Mwa 5:22; 6:9; 17:1; 1 Fal 2:4; 3:6; 2 Fal 20:3; Zab 16:8; 128:1; Mik 6:8; Mal 2:6 na wewe, ukienda mbele zangu kama alivyokwenda Daudi, baba yako, kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili, kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, 5#2 Sam 7:12; 1 Fal 2:4; 6:12; 1 Nya 22:10 ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; kama nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli.
6 #
2 Sam 7:14; 2 Nya 17:19; Zab 89:30 Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 7#Kum 4:26; 2 Fal 17:23; 25:21; Yer 7:14; Kum 28:37; Zab 44:14 basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote. 8#Kum 29:24; 2 Nya 7:21; Yer 22:8 Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? 9Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu BWANA ameleta mabaya haya yote juu yao.
10Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alizijenga zile nyumba mbili, nyumba ya BWANA na nyumba yake mfalme, 11(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya. 12Naye Hiramu akatoka Tiro kuitazama hiyo miji Sulemani aliyompa; wala hakupendezwa. 13Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli,#9:13 Katika Kiebrania ni kama ‘nyangarika au ovyo’. hata leo. 14Hiramu alikuwa amemletea mfalme talanta#9:14 Talanta moja ina uzito kama kilo 34. mia moja na ishirini za dhahabu.
Matendo mengine ya Sulemani
15 #
1 Fal 5:13; 2 Sam 5:9; Yos 19:36; 17:11; Amu 1:29 Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hasori, na Megido, na Gezeri. 16#Yos 16:10 Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani. 17#Yos 16:3; 21:22; 2 Nya 8:5 Naye Sulemani akaujenga Gezeri, na Beth-horoni wa chini, 18#Yos 19:44 na Baalathi, na Tamari ulio nyikani, katika nchi; 19na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 20Kwa habari ya watu wote waliosalia, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi, wasiokuwa wa wana wa Israeli; 21#Amu 1:21; 3:1; Mwa 9:25; Ezr 2:55; Neh 7:57; 11:3 watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 22#Law 25:39; Yer 34:14 Lakini kwa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu yeyote shokoa; ila wao walikuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maafisa wake, makamanda wa magari yake na wapanda farasi wake. 23Hao maofisa wakuu, waliokuwa juu ya kazi yake Sulemani, walikuwa mia tano na hamsini, waliowasimamia watu watendao kazi.
24 #
1 Fal 3:1; 7:8; 2 Nya 8:11; 32:5; 2 Sam 5:9; 1 Fal 11:27 Lakini binti Farao akapanda toka mji wa Daudi, mpaka hiyo nyumba yake Sulemani, aliyomjengea; kisha, aliijenga Milo.
25Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea BWANA akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za BWANA. Hivyo akaimaliza nyumba.
Shughuli za Biashara ya Sulemani
26 #
Hes 33:35; Kum 2:8; 1 Fal 22:48; 2 Nya 20:36 Tena, mfalme Sulemani akaunda merikebu huko Ezion-geberi, ulioko karibu na Elothi, pwani ya Bahari ya Shamu, katika nchi ya Edomu. 27#1 Fal 5:6,7; 10:11 Naye Hiramu akatuma merikebuni watumishi wake, wanamaji wenye kuijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani. 28#Mwa 10:2; 1 Fal 10:11; 2 Nya 8:18; Ayu 22:24; Zab 45:9; Isa 13:12 Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta#9:28 Tazama 1 Fal. 9:14. mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.
Currently Selected:
1 Wafalme 9: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.