1 Yohana 3
3
1 #
Yn 1:12,13; 16:3; 1 Yoh 5:20 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2#1 Yoh 2:28; Rum 8:17; 2 Kor 3:18; Flp 3:21; Kol 3:4; Kut 34:29 Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. 3Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. 4#Mt 7:23 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. 5#Yn 1:29; Isa 53:4; 1 Pet 2:24 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 6#Rum 6:14 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 7#1 Yoh 2:29 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki; 8#Yn 8:44 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. 9#1 Yoh 5:18 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 10Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
Pendaneni ninyi kwa ninyi
11 #
Yn 13:34; 15:12 Maana, hii ndiyo habari mliyoisikia tangu mwanzo, kwamba tupendane sisi kwa sisi; 12#Mwa 4:8 si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
13 #
Mt 5:11; Yn 15:18,19 Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia. 14#Yn 5:24; 1 Yoh 2:11 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana tunawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 15#Mt 5:21,22; Yn 8:44 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukaao ndani yake. 16#Yn 13:1; 15:13; Gal 2:20 Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 17#1 Yoh 4:20; Kum 15:7 Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18#Yak 1:22; 2:15,16 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli. 19Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake, 20ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote. 21#Rum 5:1; Ebr 4:16 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; 22#Mk 11:24 na lolote tuombalo, tunalipokea kwake, kwa kuwa tunazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. 23#Yn 6:29; 13:34; 15:12,17 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. 24#1 Yoh 4:13; Rum 8:9 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Currently Selected:
1 Yohana 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.