YouVersion Logo
Search Icon

1 Wakorintho 16

16
Michango kwa watakatifu
1 # Rum 15:25-26; Mdo 11:29; Gal 2:10; 2 Kor 8:9 Kuhusu ile michango kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo hivyo. 2#Mdo 20:7 Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; 3nami nitakapofika nitawatuma kwa barua wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu. 4Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.
Mipango ya usafiri
5 # Mdo 19:21 Lakini nitakuja kwenu, nikiisha kupita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia. 6#Rum 15:24; Tit 3:12 Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha kokote nitakakokwenda. 7#Mdo 20:2; 18:21 Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu natarajia kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia. 8#Law 23:15-21; Kum 16:9-11; Mdo 19:1,10 Lakini nitakaa Efeso hadi siku ya Pentekoste; #Mdo 19:8-10 9#2 Kor 2:12; Kol 4:3; Ufu 3:8 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
10 # 1 Kor 4:17; Flp 2:20 Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe; 11#1 Tim 4:12 basi mtu yeyote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, ili aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu. 12#1 Kor 1:12; 3:6 Lakini kuhusu Apolo, ndugu yetu, nilimsihi sana aje kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
Wasia wa mwisho na salamu
13 # Zab 31:24; Efe 6:10 Kesheni, simameni imara katika imani, iweni na ujasiri, mkawe hodari. 14Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
15 # 1 Kor 1:16; Rum 16:5 Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumia watakatifu); 16#Flp 2:29 watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha. 17Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu. 18#1 The 5:12 Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao.
19 # Mdo 18:2,18,26; Rum 16:3,5 Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao. 20#Rum 16:16; 2 Kor 13:12; 1 Pet 5:14 Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
21 # Kol 4:18; 2 The 3:17 Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. 22#Gal 1:8,9 Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha.#16:22 Maranatha: maana yake ni, Bwana wetu anakuja. 23Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. 24Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.

Currently Selected:

1 Wakorintho 16: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in