YouVersion Logo
Search Icon

1 Wakorintho 13

13
Karama ya upendo
1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2#Mt 17:20; 7:22; 21:21; Mk 11:23 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3#Mt 6:2 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu. 4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5#Zek 8:17; Flp 2:4 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6#Rum 12:9 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7#Mit 10:12; 1 Kor 9:12; Rum 15:1 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8#1 Pet 4:8 Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. 9Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; 10lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. 11Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. 12#2 Kor 5:7; Yak 1:23 Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. 13#1 The 1:3; 1 Yoh 4:16 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

Currently Selected:

1 Wakorintho 13: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in