1 Wakorintho 11
11
1 #
1 Kor 4:16; Flp 3:17 Mniige mimi kama mimi ninavyomwiga Kristo.
Kufunika kichwa
2Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea. 3#1 Kor 3:23; Efe 5:23; Mwa 3:16 Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu. 4#1 Kor 12:10; 14:1 Kila mwanamume, asalipo, au anapotoa unabii, naye amefunikwa kichwa, anaaibisha kichwa chake. 5Bali kila mwanamke asalipo, au anapotoa unabii, bila kufunika kichwa, anaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. 6Maana mwanamke asipojifunika kichwa, na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunike kichwa. 7#Mwa 1:26-27; 5:1 Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8#Mwa 2:18-23; 1 Tim 2:13 Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume. 9Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume. 10#Mwa 6:2 Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika. 11Lakini, katika Bwana si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke. 12Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu. 13Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunika kichwa? 14Je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake? 15Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi. 16Lakini mtu yeyote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu.
Matumizi mabaya katika chakula cha Bwana
17Lakini katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara. 18#1 Kor 1:10-12; 3:3 Kwa maana kwanza mnapokutanika kanisani nasikia kuna migawanyiko kwenu; nami kwa kiasi fulani naamini; 19#1 Yoh 2:19; Kum 13:3 kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu. 20Basi mnapokutanika pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana; 21kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. 22#Yak 2:5,6 Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.
Kutolewa kwa chakula cha Bwana
23 #
Mt 26:26-28; Mk 14:22-24; Lk 22:19,20 Kwa maana mimi nilipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 25#Kut 24:6-8; Yer 31:31-34; Zek 9:11 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. 26#Mt 26:29 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Kula chakula cha Bwana isivyostahili
27 #
Ebr 6:6; 10:29 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 28#Mt 26:22; 2 Kor 13:5 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. 29Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. 30#1 Kor 15:20; Efe 5:14; 1 The 5:6 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio wagonjwa na dhaifu, na watu kadhaa wamelala. 31Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa. 32#Ebr 12:5,6 Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia. 33Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutanika mpate kula, ngojaneni; 34mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake; msipate kukutanika kwa hukumu. Na hayo yaliyosalia nikija nitayatengeneza.
Currently Selected:
1 Wakorintho 11: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.