YouVersion Logo
Search Icon

Ufunuo 2

2
Ujumbe kwa Efeso
1 # Ufu 1:13,16,20 Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kulia, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. 2#1 Yoh 4:1 Ninayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wanaojiita mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; 3tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. 4Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza. 5Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu. 6#Zab 139:21 Lakini una jambo hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo mimi pia nayachukia. 7#Mwa 2:9; 3:22,24; Lk 23:43; 2 Kor 12:4; Ufu 22:2; Eze 28:13; 31:8 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.
Ujumbe kwa Smirna
8 # Isa 44:6; 48:12; Ufu 1:17; 22:13 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Haya ndiyo aneneyo yeye aliye wa kwanza na wa mwisho, aliyekuwa amekufa, kisha akawa hai. 9#Ufu 3:9; Yak 2:5; 2 Kor 11:14,15 Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. 10#Dan 1:12,14; Mt 10:28; Ufu 3:11; 2 Tim 4:8 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima. 11#Ufu 20:14; 21:8 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Ujumbe kwa Pergamo
12 # Isa 49:2; Ebr 4:12; Ufu 1:16; 19:15 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili. 13#Ufu 13:2; 3:8 Ninapajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe unalishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani. 14#Hes 22:5,7; 31:16; Kum 23:4; Hes 25:1-3; Yud 1:11 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie kikwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. 15Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. 16Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu. 17#Kut 16:14-15; 16:33-34; Yn 6:48-50; Isa 62:2; 65:15; Zab 78:24; Ufu 3:12 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Ujumbe kwa Thiatira
18 # Dan 10:6 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama muali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana. 19Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza. 20#1 Fal 16:31; 2 Fal 9:22,30; Hes 25:1,2 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. 21Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake. 22Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23#Zab 7:9; 62:12; Yer 11:20; 17:10 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wowote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine. 25#Ufu 3:11 Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja. 26#Zab 2:8-9 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, 27#Ufu 12:5 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu. 28Nami nitampa ile nyota ya asubuhi. 29Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.

Currently Selected:

Ufunuo 2: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy