Zaburi 24
24
Kuingia hekaluni
Ya Daudi. Zaburi.
1 #
1 Kor 10:26; Kut 9:29; Ayu 41:11 Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA,
Dunia na wote wakaao ndani yake.
2Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
3Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
4 #
Mt 5:8
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiweka nafsi yake katika uongo,
Wala hakuapa kwa hila.
5Atapokea baraka kwa BWANA,
Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
6Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
7 #
Hag 2:7; Mal 3:1; 1 Kor 2:8 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
Inukeni, enyi malango ya milele,
Mfalme wa utukufu apate kuingia.
8Ni nani Mfalme wa utukufu?
BWANA mwenye nguvu, hodari,
BWANA hodari wa vita.
9Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
Naam, viinueni, enyi malango ya milele,
Mfalme wa utukufu apate kuingia.
10Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?
BWANA wa majeshi,
Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Currently Selected:
Zaburi 24: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.