YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 20

20
Sala ya ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Isa 50:10 BWANA akujibu siku ya dhiki,
Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2Akutumie msaada toka patakatifu pake,
Na kukutegemeza toka Sayuni.
3Azikumbuke sadaka zako zote,
Na kuzitakabali dhabihu zako.
4 # 1 Yoh 5:14,15 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,
Na kukutimizia mipango yako yote.
5 # Isa 12:1,2; 1 Sam 17:45 Na tuushangilie wokovu wako,
Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.
BWANA akutimizie matakwa yako yote.
6Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi#20:6 Au, mtiwa mafuta. wake;
Atamjibu toka mbingu zake takatifu,
Kwa matendo makuu ya wokovu
Ya mkono wake wa kulia.
7 # Amu 7:7 Hawa wanataja magari na hawa farasi,
Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
8Wao wameinama na kuanguka,
Bali sisi tumeinuka na kusimama.
9BWANA, umwokoe mfalme,
Utuitikie siku tuitayo.

Currently Selected:

Zaburi 20: SRUVDC

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in