Zaburi 17
17
Sala ya ukombozi kutoka kwa watesaji
Ombi la Daudi.
1Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu,
Utege sikio lako kwa maombi yangu,
Yasiyotoka katika midomo ya hila.
2Hukumu yangu na itoke kwako,
Macho yako na yatazame mambo ya adili.
3 #
Ayu 23:10; Yak 3:2 Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku,
Umenichunguza usione neno;
Nimenuia kinywa changu kisikose,
4 #
Rum 12:2
Kuhusu matendo ya wanadamu;
Kwa neno la midomo yako
Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,
Hatua zangu hazikuondoshwa.
6Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7Dhihirisha fadhili zako za ajabu
Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;
Kwa mkono wako wa kulia
Uwaokoe kutoka kwa adui zao.
8 #
Kum 32:10
Unilinde kama mboni ya jicho,
Unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako;
9Wasinione wasio haki wanaonionea,
Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10Wamejawa na ukaidi,
Kwa vinywa vyao wanajigamba.
11 #
1 Sam 23:26
Wamenifuatia; na sasa wananizunguka,
Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.
12Kama mfano wa simba atakaye kurarua,
Kama mwanasimba aoteaye katika maotea yake.
13Inuka, Ee BWANA, umkabili, umwangushe,
Kwa upanga wako uniokoe nafsi yangu na mtu mbaya.
14Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu,
Watu wa dunia hii ambao fungu lao liko katika maisha haya.
Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako,
Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,
15 #
Ayu 19:26,27; Kol 1:15 Bali mimi nikutazame uso wako katika haki,
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Currently Selected:
Zaburi 17: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.