Zaburi 15
15
Nani atakaa katika patakatifu pa Mungu?
Zaburi ya Daudi.
1 #
Zab 2:5
BWANA, ni nani atakayekaa
Katika hema yako?
Ni nani atakayeishi
Katika kilima chako kitakatifu?
2 #
Zab 84:11; Isa 33:15,16 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,
Na kutenda haki.
Asemaye kweli kwa moyo wake,
3Asiyesingizia kwa ulimi wake.
Wala kumtenda mwenziwe mabaya,
Wala kumsengenya jirani yake.
4 #
Yos 9:18-20
Anayedharau waovu Machoni pake,
Bali huwaheshimu wamchao BWANA
Aliyeapa ingawa kwa hasara yake,
Hayabadili maneno yake.
5 #
Eze 18:8,9 Asiyetoa fedha yake apate kula riba,
Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.
Currently Selected:
Zaburi 15: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.