Hesabu 21
21
Nyoka ya shaba
1 #
Hes 33:40; Amu 1:16 Na Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyeishi Negebu, akasikia habari ya kuwa Israeli alikuja kwa njia ya Atharimu; basi akapigana na Israeli, akawateka baadhi yao. 2#Mwa 28:20; Amu 11:20; Law 27:28 Basi Israeli akaweka nadhiri kwa BWANA akasema, Kama wewe utawatia watu hawa mikononi mwangu kweli ndipo mimi nitaiharibu miji yao kabisa. 3#Kum 2:1 BWANA akasikiza sauti ya Israeli, akawatia Wakanaani mikononi mwao; nao wakawaharibu wao na miji yao kabisa; na jina la mahali hapo likaitwa Horma.#21:3 Maana yake ni ‘maangamizi’.
4Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia. 5#1 Kor 10:9; Zab 78:19; Kut 16:3; Mit 27:7 Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. 6#Amo 9:3,4; 1 Kor 10:9; Kum 8:15 BWANA akatuma nyoka za moto#21:6 ‘nyoka wenye sumu’. kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. 7#Zab 78:34; Isa 26:16; Hos 5:15; Kut 8:8,28; 1 Sam 12:19; 1 Fal 13:6; Mdo 8:24 Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu. 8Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. 9#2 Fal 18:4; Yn 3:14,15 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Safari kuelekea Moabu
10Kisha wana wa Israeli wakasafiri, wakapiga kambi Obothi. 11Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika jangwa lililoelekea Moabu, upande wa maawio ya jua. 12Kutoka huko wakasafiri, wakapanga katika bonde la Zeredi. 13#Hes 22:36; Amu 11:18 Kutoka huko wakasafiri, wakapanga upande wa pili wa Arnoni, ulio jangwani,#21:13 Katika makala ya Kiebrania ni ‘ambao uko jangwani’. utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori. 14Kwa hiyo imesemwa katika Kitabu cha Vita vya BWANA,
Wahebu katika Sufa,
Na bonde za Arnoni,
15Na materemko ya hizo bonde
Kwenye kuteremkia maskani ya Ari,
Na kutegemea mpaka wa Moabu.
16 #
Amu 9:21; Ufu 7:17 Kutoka huko wakasafiri kwenda Beeri;#21:16 Maana yake ni kisima. ni kisima ambacho BWANA alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.
17 #
Kut 15:1; Zab 105:2 Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu;
Bubujika Ee kisima; kiimbieni;
18 #
Kum 33:4; Isa 33:22 Kisima walichokichimba wakuu,
Ambacho wakuu wa watu wakakifukua,
Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao.
Kutoka lile jangwa wakaenda Matana; 19na kutoka Matana wakaenda Nahalieli; na kutoka Nahalieli wakaenda Bamothi; 20#Hes 23:28 na kutoka Bamothi wakaenda bondeni kwenye konde la Moabu, hata kilele cha Pisga, kielekeacho chini jangwani.
Kushindwa kwa mfalme wa Sihoni vitani
21 #
Kum 2:26; Amu 11:19 Kisha Israeli akatuma wajumbe kumwendea Sihoni mfalme wa Waamori, na kusema, 22#Hes 20:17 Nipe ruhusa nipite katika nchi yako; hatutageuka kando kwenda mashambani, wala kuingia katika mashamba ya mizabibu hatutakunywa maji ya visimani; tutakwenda kwa njia kuu ya mfalme, hadi tutakapokuwa tumetoka katika mpaka wa nchi yako. 23#Kum 29:7; 2:32,33 Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli. 24#Kum 29:7; Yos 12:1,2; 24:8; Neh 9:22; Zab 135:10; 136:19; Amo 2:9 Israeli wakampiga kwa makali ya upanga, na kuimiliki nchi yake, tangu mto wa Arnoni hata mto wa Yaboki, mpaka nchi ya wana wa Amoni; kwa kuwa mpaka wa wana wa Amoni ulikuwa una nguvu. 25Basi Israeli wakaitwaa miji hiyo yote; Israeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, katika Heshboni, na miji yake yote. 26Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni. 27Kwa hiyo, hao wanenao kwa mithali wasema,
Njoni Heshboni,
Mji wa Sihoni na ujengwe na kuthibitishwa;
28 #
Yer 48:45-46; Isa 15:4; Kum 2:9; Isa 15:1 Maana, moto umetoka Heshboni,
Umekuwa Ari ya Moabu,
Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni;
Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni.
29 #
Amu 11:24; 1 Fal 11:7,33 Ole wako Moabu!
Umeangamia, enyi watu wa Kemoshi;
Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,
Na binti zake waende utumwani,
Wamwendee Sihoni mfalme wa Waamori.
30 #
Yer 48:18,22 Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni,
Nasi tumeharibu mpaka Nofa,
Ifikiayo Medeba.
31Basi hivyo Israeli akaketi katika nchi ya Waamori. 32#Yer 48:32 Kisha Musa akatuma watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.
Kushindwa kwa mfalme wa Ogu vitani
33 #
Yos 13:12
Kisha wakageuka na kukwea kwa njia ya Bashani; na Ogu mfalme wa Bashani akaondoka apigane nao huko Edrei, yeye na watu wake wote. 34#Kum 3:2; Zab 135:10; 136:20 BWANA akamwambia Musa, Usimche; kwa kuwa nimekwisha mtia mkononi mwako, na watu wake wote, na nchi yake; nawe utamtenda kama ulivyomtenda Sihoni mfalme wa Waamori, aliyeishi Heshboni. 35#Kum 3:3,4 Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasibakize kwake mtu yeyote; nao wakaimiliki nchi yake.
Currently Selected:
Hesabu 21: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.