Marko 9
9
Kugeuka sura
1Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.
2 #
2 Pet 1:17-18
Baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao; 3mavazi yake yakimetameta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe. 4Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu. 5Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 6Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi. 7#Mt 3:17; Mk 1:11; Lk 3:22; 2 Pet 1:17; Kum 18:15; Mdo 3:22 Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 8Mara hiyo walipotazama huku na huku, hawakuona mtu pamoja nao ila Yesu peke yake.
Kuja kwa Eliya
9 #
Mk 8:30
Na walipokuwa wakishuka mlimani aliwakataza wasimweleze mtu waliyoyaona, hadi Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu. 10Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huko kufufuka katika wafu maana yake nini? 11#Mal 4:5; Mt 11:14 Wakamwuliza, wakisema, Mbona waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza? 12#Mal 4:5; Isa 53:3 Akajibu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kurejesha upya yote; lakini, pamoja na haya, ameandikiwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa sana na kudharauliwa? 13#Mt 11:14; 1 Fal 19:2,10 Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtenda yote waliyoyataka kama alivyoandikiwa.
Kuponya kwa mvulana mwenye pepo
14 #
Mt 17:14-21; Lk 9:37-42 Walipowafikia wanafunzi, waliona mkutano mkuu wakiwazunguka, na waandishi wakijadiliana nao; 15mara mkutano wote walipomwona walishangaa, wakamwendea mbio, wakamsalimu. 16Akawauliza, Mnajadiliana nini nao? 17Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu; 18na kila ampagaapo, humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze. 19Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu. 20Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu. 21Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. 22Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia. 23#Mk 11:23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24#Lk 17:5 Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutoamini kwangu. 25Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. 26#Mk 1:26 Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. 27Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama. 28Alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 29#1 Kor 7:5 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lolote, isipokuwa kwa kuomba.#9:29 Makala zingine zina ‘na kufunga’.
Yesu asema juu ya kufa na kufufuka kwake tena
30 #
Mt 17:22,23; Lk 9:43-45 Wakatoka huko, wakapita katikati ya Galilaya; naye hakutaka mtu kujua.#Yn 7:1 31#Mk 8:31; 10:32-34 Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akawaambia, Mwana wa Adamu yuaenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; na akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka. 32#Lk 9:45; 18:34 Lakini hawakulifahamu neno lile, wakaogopa kumwuliza.
Ni nani mkubwa wa wote
33 #
Mt 18:1-9; Lk 9:46-50 Wakafika Kapernaumu; hata alipokuwamo nyumbani, akawauliza, Mlishindania nini njiani?#Mt 17:24 34#Lk 22:24 Wakanyamaza; kwa maana njiani walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa. 35#Mt 20:26-27; 23:11; Mk 10:43-44; Lk 22:26 Akaketi chini, akawaita wale Kumi na Wawili akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote. 36#Mk 10:16 Akatwaa kitoto, akamweka katikati yao, akamkumbatia, akawaambia, 37#Mt 10:40; Lk 10:16; Yn 13:20 Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Mtoa Pepo Mwingine
38 #
Hes 11:27,28 Yohana akamjibu, akamwambia, Mwalimu, tulimwona mtu akitoa pepo kwa jina lako, ambaye hafuatani nasi; tukamkataza, kwa sababu hafuatani nasi. 39#1 Kor 12:3 Yesu akasema, Msimkataze, kwa kuwa hakuna mtu atakayefanya mwujiza kwa jina langu na punde baadaye akaweza kuninena kwa uovu; 40#Mt 12:30; Lk 11:23 kwa sababu asiye kinyume chetu, yu upande wetu. 41#Mt 10:42 Kwa kuwa yeyote atakayewanywesha ninyi kikombe cha maji, kwa kuwa ninyi ni watu wa Kristo, amin, nawaambia, hatakosa thawabu yake.
Majaribu ya dhambi
42Na yeyote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. 43#Mt 5:30 Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa kibutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako Jehanamu, kwenye moto usiozimika; [ 44ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 45Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, ukiwa kiguru, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika Jehanamu; [ 46ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 47#Mt 5:29 Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika Jehanamu; 48#Isa 66:24 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 49#Law 2:13 Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto. 50#Mt 5:13; Lk 14:34-35; Kol 4:6 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Muwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
Currently Selected:
Marko 9: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.