Rum 3
3
1Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini? 2#Rum 9:4; Kum 4:7,8; Zab 147:19,20; 103:7; 1 Pet 4:11Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. 3#Rum 9:6; 11:29; 2 Tim 2:13Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? 4#Zab 51:4; 116:11Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,
Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,
Ukashinde uingiapo katika hukumu.
5Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.) 6Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? 7Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? 8#Rum 6:1,2Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.
Hakuna Mwenye Haki
9 #
Rum 1:18—2:24
Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; 10#Zab 14:1-3; 53:1-3kama ilivyoandikwa, ya kwamba,
Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11Hakuna afahamuye;
Hakuna amtafutaye Mungu.
12Wote wamepotoka, wameoza wote pia;
Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13 #
Zab 5:9; 140:3 Koo lao ni kaburi wazi,
Kwa ndimi zao wametumia hila.
Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
14 #
Zab 10:7
Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15 #
Isa 59:7-8
Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao.
17Wala njia ya amani hawakuijua.
18 #
Zab 36:1
Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
19 #
Rum 2:12; Gal 3:22 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; 20#Zab 143:2; Gal 2:16; Rum 7:7kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Haki Kupitia kwa Imani
21 #
Mdo 10:43; Rum 1:17 Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; 22#Gal 2:16ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23#Rum 9:19; 5:2kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24#Rum 5:1; Efe 2:8wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; 25#Law 16:12-15; Ebr 4:16; Efe 1:7ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho#3:25Upatanisho hapa maana yake ni, Kiti cha rehema. kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; 26apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.
27 #
1 Kor 1:9,31 Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. 28#Gal 2:16Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. 29#Rum 10:12Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; 30#Kum 6:4; Gal 3:20; Rum 4:11,12kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. 31#Rum 4:3; 8:4; Mt 5:17Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
Currently Selected:
Rum 3: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.