YouVersion Logo
Search Icon

Zab UTANGULIZI

UTANGULIZI
Neno Zaburi maana yake ni “Nyimbo za Sifa”. Kitabu hiki ni mikusanyo ya namna ya mashairi mbalimbali yaliyokuwa nyimbo za kumsifu na kumwabudu Mungu na kuimarisha katika imani.
Zaburi hizi zilitungwa kishairi na watu kadhaaa wa nyakati na mazingira tofauti. Ziliimbwa na watu wote walioishi nyakati mbalimbali. Baada ya kuzitumia kwa muda mrefu zilikusanywa zikafanywa vitabu vitano. Kila kitabu kilihitimishwa kwa maneno ya kumsifu Mungu (41:13; 72:18-19; 89:52; 106:48 na 150). Baadaye vitabu hivyo viliunganishwa vikawa kitabu hiki cha Zaburi. Zaburi ya 150 ni hitimisho la Kitabu cha Tano na vile vile ni kilele cha sifa kwa kitabu chote cha Zaburi. Umuhimu wa Zaburi hautokani na umahiri wa kishairi bali mwelekeo wa kila hisia ndani ya roho ya mtu binafsi au jamii ya waaminio ielezayo uhusiano ulioko kati yao na Mungu.
Kitabu hiki chaeleza hisia za hali za watu binafsi (3, 54, 75), na jamii kwa ujumla: kama furaha, msaada, ukombozi, ulinzi na kumwomba Mungu atoe rada kwa adui. Kuna ibada za hadhara, sikukuu za hekaluni (38) na sherehe maalumu kwa ndoa (45), kumtawaza mfalme na kuadhimisha ushindi (2; 18; 110). Kwa kuwa Zaburi hugusia sehemu zote za maisha, taifa la Mungu wakati wote walitilia maanani Zaburi.
Baadhi ya Zaburi zimetaja watunzi wake. Mfalme Daudi anatajwa kuwa mtunzi wa Zaburi kama 73. Wengine ni Asafu (50; 73–78) Hemani (88) Ethani (89), Sulemani (72, 127), na Musa (90).
Kitabu hiki kimegawanywa katika mafungu makubwa matatu: kwanza ni za kumtukuza na kumsifu Mungu, utendaji wake ulimwenguni wote na katika kuliongoza taifa lake (8; 19; 29; 107). Vile vile zatukuza Sayuni ambapo Yerusalemu umejengwa na ndani yake kuna maskani ya Mungu (46; 48; 76; 84; 122). Kutoka Yerusalemu Ufalme wa Mungu utatangaziwa ulimwengu (33; 47; 87; 93; 96–100; 103–106; 113–114; 117; 135–136; 145–150).
Pili ni za maombi na maombolezo. Zaburi zinamwelekea Mungu na kumweleza hali yao ya taabu, adha na huzuni walizo nazo. Imetumiwa mifano ya vilindi vya maji, lindi la mauti, Jahanamu na wanyama wakali ili kueleza hali ya sononeko ilivyo (4–5; 11; 16; 22–23; 26; 42–44; 55–57; 62–63; 121; 125; 130–131). Maombolezo ya mtu mmoja mmoja (3, 7, 13, 25, 51) na ya jamii hasa kwa ajili ya maafa ya kitaifa (44, 74).
Tatu ni za kushukuru Mungu. Taifa lilishukuru kwa kuwa limekombolewa toka kwa maafa fulani, kuvuna mavuno mengi na kwa ajili ya fadhili (2; 18; 20–21; 31–32; 34; 40; 45; 65–68; 92; 116; 118; 124; 129; 139; 144). Shukrani za mtu binafsi kuhusu kujibiwa aliyoomba na kuokolewa (22; 30; 69; 140).
Yaliyomo:
1. Kitabu cha Kwanza, Sura 1–41
2. Kitabu cha Pili, Sura 42–72
3. Kitabu cha Tatu, Sura 73–89
4. Kitabu cha Nne, sura 90–106
5. Kitabu cha Tano, Sura 107–150

Currently Selected:

Zab UTANGULIZI: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy